Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James ametoa pongezi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kufanya vizuri kwenye suala zima la utekelezaji wa mkataba wa Lishe. Mhe. James ametoa pongezi hizo katika kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa robo ya pili 2024/2025 kilichofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya iliyopo Mawelewele Januari 16, 2025.
Katika taarifa iliyowasilishwa mbele ya kikao cha tathmini ya afua za lishe, inaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imefanya vizuri kwenye kadi ya alama mkataba wa lishe ngazi ya jamii ambapo kila kipengele kina rangi ya kijani.
Sanjari na hayo Mhe. Kheri ameipongeza Iringa DC hasa kwenye eneo la utoaji wa fedha za afua za lishe ambapo kwa robo hii zaidi ya milioni 31 zimetolewa ambazo ni 162.8% sawa na shilingi 2,745.3 kwa kila mtoto.
Aidha Mhe. Mhe. Kheri amekumbusha kuwa Iringa DC ina nafasi ya kufanya vizuri si tu kwenye suala la lishe bali kwenye maeneo yote ikiwemo mbio za Mwenge wa Uhuru kwani wana nafasi ya kujifunza kwa wengine wanao wazunguka ikiwemo Halmashauri za Jirani.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Steven Mhapa amesisitiza juu ya utoaji wa elimu ya sumu kuvu, sumu ambayo imekuwa tishio kwa jamii kutokana na uhifadhi wa chakula usio sawa wa chakula na kushauri kuwa badala ya mtu mmoja wa Idara ya Kilimo kufanya hiyo kazi maeneo yote, wajengewe uwezo watu wengine wanaoweza kutoa hiyo elimu ili kuunda timu itakayorahisisha kuyafikia maeneo mengi.
Kikao cha tathmini ya mkataba wa lishe kimeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James ambacho kimehudhuriwa na Maafisa lishe wa Halmashauri, Wakuu wa Idara na vitengo katika Halmashauri na watendaji wa kata ambao wapo mstari wa mbele kwenye usimamizi wa shughuli mbalimbali za afua.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa