MKUU WA WILAYA YA IRINGA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy ametoa pongezi hizo alipokuwa katika Mkutano wa Tathmini ya Maendeleo ya Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kilichofanyi kakatika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo 24.03.2023.
Mhe Kessy amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka kipaombele kwenye sekta ya elimu hasa kwenye ujenzi wa miundombinu ya shule ambapo fedha nyingi zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati yake.
Aidha Mhe. Kessy amewapongeza wadau wengine wa elimu kwa michango yao kwenye sekta hii “Nachukua fursa hii kuwapongeza wadau wote wa maendeleo ya elimu kwa namna mnavyotoa michango yenu kwenye sekta ya elimu ambapo kwa sehemu kubwa mmetoa michango katika kutatua changamoto mbalimbali za elimu zikiwemo upungufu wa madarasa, madawati, maji, kuwasaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu hasa wasichana, lakini pia upungufu wa matundu ya vyoo, ujenzi wa mabweni hasa ya wasichana pamoja na misaada mingine mingi mnayotoa katika sekta ya elimu”.
Amewataja baadhi ya wadau hao ambao ni Wahe. Wabunge na madiwani, NMB bank, CRDB bank, CAMFED, World Vision Tanzania, Lyra Africa, Afya Plus, Focus Development, Shafa Agro Limited, DESWOS, SEED, ANUE, IBO, A. L. M, ASAS, AMELIA’S LTD, Eng. Daniel Kindole, Mohamed Mt. Huwel na Fu Yong.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Wilaya amewaasa walimu, watendaji, maafisa elimu, walezi na wazazi kusimamia nidhamu ya wanafunzi ambapo katika zama hizi kuna tabia mbovu sana zimeibuka hivyo ni jukumu letu sote kuwaangalia watoto kwenye mienendo yao.
Kwa upande wa taaluma Mhe. Kessy amesema kama ilivyo kauli mbiu ya mkutano huu, “Vunja Mnyororo wa wa Utapiamlo kwa kuhakikisha Mwanafunzi anapata Lishe Bora awapo Shuleni ili kuongeza Ufaulu” basi tutimize wajibu wetu wa jambo hili kwa kutoa chakula shuleni.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Stephen Mhapa ametoa pongezi kwa watumishi wote, Wahe. Madiwani, wadau wa Elimu na Mkurugenzi mtendaji (W) kwa kufanya kazi vizuri, pia walimu kwa kazi yao njema hasa wakati wa utekelezaji wa miradi ya ujenzi,
Akitoa salamu za kamati ya Huduma za jamii (Elimu, Afya na Maji) Mhe. Felix Waya amesema, wanatambua mchango wa walimu pamoja na changamoto zinazowakabili lakini wamekuwa mstari wa mbele kufanya kazi na kuomba kuwa ikiwezekana bajeti ya mitihani iongezwe ili watoto waweze kujipima mara kwa mara.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri amepongeza kazi nzuri na kubwa anazozifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye miundombinu ya shule na barabara ambapo imeongeza hamasa kwa wanafunzi kupenda shule.
Vilevile Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Amesema, “Kutokana na umuhimu wa sekta hii, tumeona tufanye tathmini kwa lengo la kuona maendeleo ya elimu na kujipima kutokana na malengo tuliyojiwekea mwaka jana.
Naye Afisa Elimu(W) Ndg. Mwenekitete akisoma taarifa za maendeleo ya elimu amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina shule za sekondari 49 ambapo 34 ni za serikali na 15. Katika tathmini kuna shule zilizofanya vizuri na chache kufanya vibaya kwenye baadhi ya maendeo ambapo waliofanya vizuri walipatiwa vyeti vya pongezi na waliofanya vibaya walipwa bango la shule dhaifu kitaaluma. Aidha kuna shule sita ambazo zimepatiwa zawadi ya mbuzi ambazo ni shule sita kama ifuatavyo; St. Mary’s Ulete, Migoli sekondari, Kalenga sekondari, Ifunda tech, kiamaiga, na Lipuli sekondari.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa