Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy leo tarehe 18/07/2023 ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Msingi Itunundu. Shule hii inajengwa kwa mradi wa Boost ambapo serikali imetoa kiasi cha Tshs. 347,500,000 kwaajili ya kazi hiyo
Pia Mhe. Kessy ametembelea eneo ambalo itajengwa Shule Mpya ya Sekondari ya Mboliboli iliyopo kata ya Mboliboli katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Mradi huu umeletwa kwa program ya SEQUIP, ambao utatumia kiasi cha Milioni 583 hadi kukamilika kwake
Katika ziara hii Mhe. Kessy amewaomba wananchi wa kata ya Mboliboli kutoa nguvukazi ikiwa ni pamoja na kusafisha eneo la mradi, na kuchimba msingi ili ili ujenzi huo uanze mara moja.
Kwa upande mweingine Mhe. Kessy ametembelea na kukagua kazi inayoendelea ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA cha Pawaga ambapo kazi inaendelea.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa