Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amefanya ziara katika tarafa ya Isimaniambapo amekagua miradi ya maendeleo, kuongea na walimu sanjari na kuongea na wananchi kupitia mkutano wa hadhara na kutatua changamoto ya mgogoro wa ardhi Agosti 20, 2024.
Katika miradi ya maendeleo Mhe. Kheri, amekagua ujenzi wa maabara, chumba cha upasuaji, nyumba ya mtumishi na ujenzi wa vyoo vya kisasa ambapo miradi yote hii ipo katika hatua za mwishoni kwa ajili ya ukamilishwaji. Mhe. Kheri amepongeza kazi kubwa iliyofanyika na inayoendelea kufanyika na kutoa wito wa kutunzwa kwa miundombinu husika
Mhe Kheri amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya fedha zilizoletwa hasa kwenye jengo la upasuaji ambapo tayari vifaa vyote vinavyotakiwa vimeshatolewa na huduma zimeanza kutolewa.
Kwa upande mwingine Mhe. Kheri chanzo cha maji kilichopo Izazi kabla ya kuwa na wasaa wa kuongea na walimu wa shule mbalimbali za kata ya izazi na baadaye kuongea na walimu wa shule za kata ya Migoli.
Aidha, katika kijiji cha Migoli Mhe. Kheri amefanya mkutano na viongozi mbalimbali wa dini, kusikiliza mgogoro wa mipaka kati ya kijiji cha Mbweleli na Makatapola ambapo baadaye jioni amefanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Migoli na maeneo ya jirani kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua.
“Iringa Bora itajengwa kwa Umoja na Uwajibikaji”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa