Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James amefanya ziara katika Tarafa ya Kiponzelo Agosti 21, 2024 ambapo ameweza kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo shule la sekondari Lumuli na Lyandembela, ukarabati wa miundombinu ya afya katika Zahanati ya Lumuli, kukagua ujenzi wa tanki la maji Ifunda, kisha kuongea na watumishi na baadaye kuongea na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Ifunda.
Akizungumza na wananchi amepongeza juhudi za serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi inayoendelea na kuhimiza viongozi wa ngazi ya Halmashauri na taasisi husika kusimamia utekelezaji wake ili kuhakikisha kuwa miradi inakamilika kwa ubora.
“Kazi nzuri inayofanywa kwa faida ya wananchi lazima isimamiwe. Hizi fedha zinazoletwa ni za walipa kodi ambao ni sisi wenyewe hivyo lazima tuzingatie thamani ya fedha katika mradi kwani mafundi ama watu wengine wanapoharibu hawaharibu mali ya shule bali wanaharibu mali yetu” amesema.
Aidha Mhe. Kheri amekemea suala la wananchi kuchangishwa michango hata wakati ambao serikali imesha leta fedha za kutosha kwa ajili ya mradi husika na kuongeza kuwa wananchi wachangie michango kwenye miradi yao wanayoiibua kwa makubaliano yao na sio kwenye miradi ambayo tayari serikali imeshatenga fedha inayotosha.
Kwa upande wake Mhe Diwani wa kata ya Lumuli kwa niaba ya wananchi ametoa shukrani kwa miradi mingi iliyoletwa kwenye sekta ya elimu na afya na kuahidi kutoa ushirikiano na kuisimamia ipasavyo.
Mhe. Kheri pia amezungumza na wananchi ambapo amesisitiza juu ya utawala wa sharia, uwazi, usawa, uwajibikaji, umoja na mshikamano kwa wananchi wote na kupata nafasi ya kuwasikiliza wananchi juu ya kero mbalimbali na kuzitafutia utatuzi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa