Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James Aitaka Kamati ya Mbio za Mwenge Kukamilisha Maandalizi
Ameyasema hayo Mei 07, 2024 wakati akikagua miradi na njia itakayopita Mwenge wa Uhuru. Amesisitiza kushirikishwa kwa Watendaji Kata na vijiji, Madiwani, Wenyeviti wa Vijiji, ili wananchi wajitokeze kwa wingi wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza na Kamati hiyo Mhe. Kheri, ameipongeza Kamati kwa kuchagua miradi ambayo inaendana na vigezo vya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu na kufurahishwa na ratiba iliyoandaliwa.
Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na Utunzaji wa mazingira, elimu vyumba vya madarasa na mabweni ya wanafunzi, daraja na vituo vya huduma za afya ambavyo vinatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Naye Mratibu wa Mwenge Mkoa Ndugu Stephen Sanga amepokea maelekezo yote na kuahidi atayafanyia kazi kwa kushirikiana na Mratibu wa Mwenge Wilaya Bi. Sakina Mgaya.
Mwenge wa Uhuru 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa unatarajiwa kupokelewa mnamo mwezi Juni 26, 2024 ukitokea Halmashauri ya Mji Mafinga na baadaye kukabidhiwa Mkoani Dodoma. Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 "Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu".
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa