“WATENDAJI TOENI ELIMU KWA JAMII YENYE KULETA TIJA YA MAPAMBANO DHIDI YA UDUMAVU” AAGIZA MH. MOHAMED HASSAN MOYO DC IRINGA.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Mohamed Hassan Moyo amewaagiza watendaji,Wajumbe na Wadau wa masuala ya lishe kujitoa muhanga katika kutokomeza udumavu na utapiamlo katika maeneo yao ili kutokomeza kabisa tatizo hilo.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha robo ya nne cha Aprili - Juni kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisini kwake Julai 7, 2021 kikao ambacho ni cha tathimini ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya jamii.
Mh. Moyo amewataka washiriki wa kikao cha kamati ya lishe kuhakikisha wanazingatia lishe bora kwa watoto na wakina mama wajawazito kabla ya kujifungua ili kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
"Natamani kikao kijacho cha tathimini nione mabadiliko na nipate muhtasari wa utekelezaji wa maadhimio ulipofikia hasa katika kuhamasisha wananchi kupambana dhidi ya udumavu kupitia Elimu iliyotolewa na matokeo yake" alisema Mh. Moyo
Naye, Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bi. Tiliza Mbulla alieleza historia ya mkataba na tatizo la udumavu na utapia mlo amesema tatizo hilo limekuwa likiathiri zaidi uchumi wa kaya na taifa lakini kupitia uwezo duni wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi kwa muathirika.
Bi.Mbulla alitoa rai wa wajumbe wa kamati ya Lishe kuwa na taarifa sahihi za tatizo la watu wenye udumavu katika Kata zao ili kurahisisha kuwafikia waathirika nan a kupata utatuzi wa haraka wa changamoto hiyo.
Kabla ya kufunga kikao hiko Mh.Moyo amewashauri wajumbe kwenda kuhamasisha shughuli za kilimo katika maeneo yao husani kilimo chenye tija ikiwemo kilimo cha zao la maparachichi ambacho mbali na kutumia kama tunda wanaweza kuuza na kuongeza pato katika kaya na jamii zao kwa ujumla.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa