DC-Iringa aja na ziara ya ulipo nipo itakayoanza mapema Septemba mwaka huu,toa kero na changamoto.
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa -DC)
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Mohamed Hassain Moyo anatarajia kuanza ziara ya kusikiliza kero mapema mwezi Septemba na anaanza na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Mh.Moyo amesema hayo Ofisini kwake leo Agosti 16,mwaka huu wa 2021 na kubainisha kuwa katika ziara hiyo ataambatana na Wataalam wa Idara zote kutoka Halmashauri na migogoro na kero nyepesi zitapaiwa uvumbuzi wa hapo kwa hapo.
“nimeamua kuwafuata wananchi hasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa jinsi ilivyo kuna uwezekano wapo wananchi wanapata changamoto au wanakero lakini wanashindwa kunifikia nimeamua kuwafuata,kusikiliza na kutatua kero zao na ziara nimeipa jina la ulipo nipo,toa kero na changamoto,sema ukweli na sio majungu”alisema Mh. Moyo.
Kuhusu suala la chanjo Mh.Moyo amesema atajipanga na wataalam wa afya wa Halmashauri ili katika ziara hiyo waweze kuwa na dawa na kwa wananchi watakaokuwa tayari kwa hiyari yao watapatiwa chanjo hiyo.
“Naamini wapo baadhi ya wananchi wanahitaji huduma hii lakini umbaali kutoka katika makazi yao mpaka kufika eneo la kituo cha kutolea huduma imekuwa changamoto sasa kwa waliotayari na kwahiyari ataweza kupata huduma hii katika ziara yangu ninayotarajia kuanza mwezi Septemba ambayo ni ziara ya Kijiji kwa Kijiji awali nilifanya ziara ya Kata kwa Kata”alisema.
Nataka wananchi wote wenye kero na changamoto kujitokeza kuzungumza kero zao na chaangamoto zao ila wasimuonee mtu wala wasifanye majungu.
“Mh. Rais ameniteua kuja kuwatumikia wananchi ikiwemo kusikiliza na kutatua kero zao na sio kuja kukaa ofisini ili viongozi wa kitaifa wakipita wakutane nazo”alisema Mh.Moyo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa