DC-Moyo atoa rai, Wananchi nendeni katika Zahanati na Vituo vya Afya mkapate chanjo ya UVIKO-19.
Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Msingi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Mohamed Moyo ametoa rai kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa UVIKO-19 ili kuimarisha kinga za miili yao dhidi ya ugonjwa huo.
Amesema hayo Novemba 30 katika ukumbi wa siasa ni kilimo ambapo alikuwa akifanya kikao cha mwezi cha Kamati hiyo ambapo taarifa ya Utekelezaji wa zoezi la Utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Akitoa taarifa ya mwenendo wa chanjo hiyo Mratibu wa chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw. Sospeter Tiyara amesema kwa sasa muitikio ni mkubwa ukilinganisha na awamu ya kwanza ambapo wananchi wengi walikuwa hawana uelewa wa kutosha sambamba na kushibishwa taarifa potofu kutoka katika baadhi ya mitandao ya kijamii.
Hadi kufikia 29 Nov 2021 Halmashauri ya Wilaya imetumia dozi 4572 sawa na 68.58% ambayo jumla ya wateja waliochanja aina ya JANSSEN na awamu ya pili ya chanjo aina ya SINOPHARM kati ya dozi 6667 zilizopokelewa kutoka katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa.
“Mkuu wa Wilaya katika ziara yake ya ulipo nipo alikuwa akitoa elimu na uhamasishaji wa kuchanja katika kila kijiji alichopita ambapo alikuwa akifanya mikutano ya hadhara,lakini pia Mbunge wa Jimbo la Ismani Mh.William Lukuvi na Viongozi mbalimbali wa kisiasa walifanya uhamasishaji wa zoezi la chanjo ya Uviko-19”alisema Bw.Tiyara.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa