World Vision na SOS wafanikisha uzinduzi wa Baraza la Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Iringa
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano, Iringa-DC)
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela leo Oktoba 20 amezindua Baraza la watoto la Halmashauri ya Wilaya ambalo lina jumla ya wajumbe 56 ambao ni wawakilishi kutoka Mabaraza ya Kata.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mh.Kasesela amesema Mabaraza hao yatumike kufikisha sauti kwa jamii na wahusishwe katika kutoa mawazo yao hasa katika vikao na mikutano ya vijiji na Kata ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kuweza kujitetea.
“Baadhi ya Wazazi wamekuwa wakiwachukia watoto bila sababu,ni tabia ambayo baadhi ya wazazi wanayo ya kutolipa uzito suala la malezi kwa watoto nah ii pia,inachangia katika makuzi ya motto hupelekea hata udumavu kutokana na mtoto kukosa upendo wa wazazi wake huku wengine wakijikita katika ulevi ulio kithiri”alisema.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mganga Mfawidhi Dkt Samuel Marwa amewapongeza wadau wa World Vision na SOS kwa kujitoa kwao katika kuunga mkono jitihada na juhudi za Halmashauri katika masuala ya watoto kwani sio tu katika kufanikisha baraza hilo bali wamewezesha watoto waishio katika mazingira duni kupata bima yay a Afya kwa kaya zaidi ya elfu moja.
“Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji napenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa wadau wote wanaoshirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kufanikisha masuala mbalimbali ya kijamii husasani katika sekta ya Elimu,Afya na Uatawi wa Jamii”alisema Dkt.Marwa
Naye Mwenyekiti wa Baraza la watoto la Halmashauri ya Wilaya mwanafunzi wa shule ya Sekondari Tanangozi Theresia Msemwa amewaomba wazazi wawaruhusu watoto waweze kushiriki katika masuala yanayohusu watoto ilikuweza kukua kwa kujitambua na kuweza kijisimamia.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa