Mkuu wa Wilaya aongoza Harambee ya magodoro shule ya Sekondari Ilambilole.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa –DC)
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela ameongoza Harambee ya kuchangia Magodoro ya shule ya Sekondari Ilambilole wakati alipokuwa mgeni Rasmi katika makabidhiano ya Bweni la Wasichana lililojengwa na Shirika Lisilo la kiserikali la Lyra lenye thamani ya shilingi 178,800,000/=ambapo shirika la Lyra lilichangia 86% sawa na shilingi 162,486,721, nakiasi kilichobakia kilichangiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo.
Mh. Kasesela amelipongeza Shirika la Lyra na Viongozi wa Kata na Jimbo la Ismani kwa kujitoa sana kwa Wananchi wao lakini pia,kwa wadau wa maendeleo ambao wamewezesha sana kujengwa kwa Bweni hilo wakiwemo wananchi,Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na Alif Abri na Feisal Abri ambao wamechangia maeneo mengi katika jamii inayowazunguka.
Akisoma taarifa fupi kwa Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Lyra Bi. Roselyn Mariki amesema shirika hilo limeshajenga mabweni kumi na moja (11) ambayo yanalenga kuwasaidia wananfunzi wa kike ambao wapo katika hatari kubwa ya kupata ujauzito kutokana na kutembea umbali mrefu lakini pia wanafunzi wananoishi katika maisha magumu na hatarishi.
Bi.Mariki alielezea kazi nyingine zinazofanywa na Shirika hilo kuwa ni mradi wa Imarika Kijana ambao unalenga kuwasaidia vijana walio vijijini ambao kwa sababu moja au nyingine hawakufanikiwa kuendelea na masomo ama kupata ajira, Shirika la Lyra limeshatoa mafunzo kwa vVijana 210 kati ya hao 40 wamewachukua ili kusaidia kutoa elimu ya uwezeshaji kwa vuijana wengine.
“Mgeni rasmi mpaka sasa kuna vikundi 11 vya Vijana vya Hisa vilivyoanzishwa vikiwa na na mitaji na akiba ya chini ya shilingi elfu 50 na kwa sasa vina jumla ya shilingi milioni is20 zikiwa ni mitaji na akiba”alisema.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Bi.Saumu Kweka aliwaasa wanafunzi kutumia fursa ya uwepo wa Bweni hilo kujikita katika kujisomea ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao kwani kiongozi bora lazima awe na elimu nzuri na kuwahakikishia kwamba yeye kwa nafasi yake na kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji watachangia magororo Matatu yenye thamani ya shilingi 165000/.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa