Msemaji Mkuu wa Serikali Azungumza na Vyombo vya Habari
Msemaji Mkuu wa Serikali Ndugu Mobhare Matinyi, amefanya mkutano Mkoani Iringa ili kuzungumza na vyombo vya Habari Mkoani humo Februari 01, 2024.
Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa ukiwa na lengo la kutoa nafasi kwa wananchi kujua Serikali inafanya nini.
Ndugu Matinyi amesema, “Rais na Serikali yake wanahakikisha Watanzania wanawasikia na kuwafikia katika kukata kiu ya maendeleo wanayoyatarajia. Fedha nyingi zimetolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi na kwamba mafanikio yameonekana kama ujenzi wa shule mpya za Msingi na Sekondari, Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali na vifaa vyake, yote haya wananchi wanatakiwa kujua”.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendengo akitoa taarifa ya Mkoa ambayo imetaja kila kona kuanzia ukubwa wa Mkoa na usalama wake amesema, “shukrani za pekee ziende kwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Awamu ya Sita kwa kuongoza Serikali hii yenye kila aina ya mafanikio”.
Mheshimiwa Dendego ameendelea kusema, “tumepokea mabilioni ya fedha kwa Mkoa wa Iringa ili tuweze kutekeleza miradi katika Nyanja mbalimbali, na wananchi wamepokea kwa mikono miwili. Ujenzi wa shule mbalimbali, ujenzi wa zahanati, vituo vya Afya, Hospitali, barabara, maji na miundombinu ya umwagiliaji, katika Wilaya zote za Iringa”.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Iringa wamepata nafasi kila mmoja kuzungumzia Halmashauri yake jinsi ilivyonufaika na utekelezaji wa miradi mbalimbali. Katika Mkutano huo alikuwepo Wakili Bashir Paul Muhoja, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Lain Kamendu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Charles Fuss, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Ayoub Kambi, Mkurugenzi wa Mji Mafinga, na Kastori Msigala, Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa.
Wakurugenzi hao wamemshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali wananchi wake.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa