“Mvua ni Baraka Lakini Zinaleta Madhara Pale Zinapokuwa Nyingi Kupita Kiasi” – Mheshimiwa Mhapa
Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa alipokuwa anatoa taarifa ya hali ya Halmashauri katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Siku ya Kwanza kwa Robo ya Kwanza Julai – Septemba, 2023/2024 ambapo umefanyika Desemba 07, 2023 na utaendelea hadi Desemba 08, 2023.
Mheshimiwa Mhapa amesema, “Mvua zimeanza kunyesha kwa kasi, hivyo tuwatangazie wananchi na wakulima wote kwenda kujisajiri katika mfumo ili waweze kupata mbole ya ruzuku kutoka Serikali Kuu”.
Mheshimiwa Mhapa ameendelea kusema kuwa, “Pamoja na kwamba mvua ni Baraka lakini zinakuja na kuleta madhara. Wenzetu wa Kata ya Migoli wamepata maafa ya mafuriko na kusababisha baadhi ya Kaya kukosa makazi na chakula, hivyo tutoe tahadhari za kiusalama kwa wananchi wetu. Pia Kata ya Idodi kuna watoto wawili wamefariki baada ya kutumbukia katika shimo lenye maji mengi yaliyosababishwa na mvua. Nawaomba wananchi wanapotaka kuvuka kwenye makorongo yenye maji, muwe waangalifu sana”
Bada ya taarifa hiyo, wajumbe wa Baraza hilo (Madiwani wa Kata) waliweza kuwasilisha taarifa kutoka kwenye Kata zao, ambapo zimebeba mafanikio na changamoto, na kwamba baadhi ya changamoto zilipatiwa majibu ya moja kwa moja, na nyingine Mwenyekiti alizipokea na kwenda kuzifanyika kazi.
Aidha Mheshimiwa Mhapa amewataka wajumbe wa Mkutano huo kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusema kuwa, wanahitaji Watendaji wa Kata na Vijiji waongezwe kwa kutoa ajkwani vijiji vingi havina watendaji, maji safi na salama kwenye Taasisi, mbolea ya ruzuku ije kwa wakati, uhamisho wa watumishi hasa walimu wanaobadilishana kwani imekuwa tatizo, kukatika kwa mawasiliano ya barabara kutokana na mvua nyingi, uchakavu wa majengo ya shule za msingi na umeme kwenye baadhi ya vitongoji na vijiji.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa