Mvua Kubwa Zaleta Madhara Shule ya Sekondari Weru
Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, imesababisha madhara ya kujaa kwa maji katika shule ya Sekondari Weru iliyopo Kata ya Ulanda. Kamati ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Januari 20, 2024 imetembelea shule hiyo na kujionea madhara yaliyojitokeza katika eneo hilo.
Kwa kushirikiana na Diwani wa Kata hiyo Mheshimiwa Philemon Temaigwe, Mtendaji wa Kata, Mwenyekiti wa Kijiji cha Weru na wananchi, wametoa maamuzi ya kuchimba mfereji mkubwa ambao utakakinga maji kutoinigia katika viwanja vya shule, na kuyasafirisha mbali na eneo hilo.
Shule hiyo ni mpya ambayo imejengwa kwa mpango wa SEQUIP na kwamba imeanza Kidato cha Kwanza mwaka huu 2024. Hadi Sasa wanafunzi walioripoti Kidato cha Kwanza kwa mwaka 2024 ni 112 (Wav 50, Was 62) kati ya waliopangwa ni 148.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa