“Mwanamke Akiwa wa Hovyo, Baba Anakuwa Hovyo Zaidi” – Mhe. Mhapa
Kauli hii imetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa, ambapo alikaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika Kiwilaya Machi 06, 2024 katika Kata ya Ulanda Kijiji cha Ibangamoyo viwanja vya Shule ya Sekondari Kalenga.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka tangu kuanzishwa kwake. Katika maadhimisho hayo Wanawake husherehekea kwa namna mbalimbali na pia hukumbushana na kufundishana stadi za maisha.
“Mwanamke ni kila kitu katika familia, mama akilegalega basi kwa asilimia kubwa familia itayumba. Baba peke yake hawezi kulea na kutunza familia. Mama akiwa wa hovyo basi Baba atakuwa hovyo zaidi”. Amesema Mheshimiwa Mhapa.
Mheshimiwa Mhapa amewasisitiza Wanawake hasa Wakristo kusoma aya ya kwenye Biblia ya Petro 1:1-2. Hii itasaidia kila Mwanamke kujikumbusha wajibu wake katika familia.
Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Bi. Rehema Mohamed amesema, “Sisi Wanawake tunasomwa kama barua, basi tusomwe vizuri ili jamii izidi kutuamini na kuiga mifano kutoka kwetu. Kila mafanikio ya Mwanaume yeyote nyuma yake kuna Mwanamke”.
Bi. Rehema ameendelea kusema, Mwanamke anatakiwa kumuombea sana Mwanaume kila anapotoka na kwenda kutafuta, kadhalika na familia nzima, kwani mama ndiye kiongozi wa familia. Kauli mbiu hii inaakisi kuwa mwanamke ni mpambanaji, hivyo jamii inapaswa kumuamini”.
Pamoja na mambo mengi yaliyoongelewa siku hiyo, kulikuwa na burudani za kutosha na kukonga nyoyo za watu.
Katika siku hii, Kauli Mbiu ya mwaka huu inasema “Wekaza kwa Mwanamke Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa