Mwananchi Digital Wafuatilia Taarifa Juu ya Umuhimu wa Bwawa la Mtera
Bwawa la Mtera ni muhimu sana kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na wananchi wake kwa ujumla, na hata Wilaya za jirani za Mpwapwa na Chamwino kwa Jiji la Dodoma.
Siku za hivi karibuni kumekuwapo na upungufu wa upatikanaji wa samaki katika bwawa hilo ambao unatokana na sababu mbalimbali.
Mwananchi Digital wameweza kufanya ufuatiliaji juu ya ukosefu wa samaki katika bwawa hilo leo uwepo wa mamba na viboko wanaotishia wananchi na baadhi ya Wavuvi kutelekeza familia zao baada ya kukosa kipato walichokuwa wanategemea baada ya kuvua samaki Machi 11, 2024,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya Ndugu Robin Gama ameweza kutolea ufafanuzi juu ya jambo hilo na kwamba ufuatiliaji juu ya utunzaji wa bwawa hilo bado unaendelea.
Aidha, Kaimu Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ameweza kufafanua juu ya umuhimu wa kuvua samaki wanaohitajika katika soko, pia Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii ameweza kuzungumzia kuhusu baadhi ya wavuvi waliotelekeza familia na kuwahusia wanawake kujitokeza katika fursa mbalimbali na mikopo ili waweze kukidhi mahitaji yao na watoto, na Kaimu Afisa Maliasili Ndugu Charles Mdendemi ameweza kutoa jinsi gani wavuvi waweze kuvua samaki kwa njia salama ili wasipate madhara ya kukamatwa na mamba na viboko.
Makala hiyo itawajia mara tu itakapokuwa tayari, kwani kwa sasa ipo kwenye mchakato.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa