Mwanasheria Iringa Dc Awapa Madini ya Kiutumishi Watumishi wa Kata ya Idodi
Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mathod Msokele amewataka Watumishi kuwa makini katika utendaji kazi wao wa kila siku kwa kufanya kazi kwa wajibu na haki ili kufikia malengo ya serikali na malengo yao binafsi.
Kazi inapaswa ifanywe kwa weredi na kupenda kurudia kazi, kuihakiki kama iko sawa kabla ya kuituma mahali popote, hii itasaidia kutambua makosa ambayo yanaweza kuwa yamejitokeza na kupelekea kukutwa na hatia, kadhalika kufanya kazi kwa kujituma ili kuepusha mogorogoro inayoweza kuibuka kati ya Muajiri na Mtumishi.
Ameyazungumza hayo ikiwa ni siku ya pili ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika katika Kata ya Idodi alipokuwa akiwasilisha mada ya Wajibu wa Mtumishi wa Umma pia amesisitiza kufanya kazi kwa ubunifu, kwani kufanya kazi kwa mazoea kunapelekea kuzoeleka na hivyo makosa kuwa ni yale yale kila siku.
"Ubunifu ni kutumia mawazo yako ili kujiendeleza kiufanisi zaidi, na ili uweze kujiendeleza vizuri hayo mawazo na yalete ufanisi mzuri zaidi hakikisha unatumia taaluma yako vizuri na uzoefu ulionao kuboresha zaidi, kila siku ya Mungu hakikisha unakuwa mpya".
Usipokuwa mbunifu utakuwa unatumia kila siku mambo ya zamani na kila siku watakuwa wanakuona ni yule yule hatimae utaishia kulaumu tu na kuyaona mazingira ya kazi uliyopo hayastahili na kuanza kudai kuhamishwa bila sababu ya msingi.
Utakuwa unakimbilia kuomba uhamisho kila siku kwa sababu wewe mwenyewe kwanza sio mbunifu ambae unafikiri mambo mapya kila siku na ili wakuone mpya, Ameongeza.
Pia amewataka Watumishi wa Umma kuwa na shauku ya kazi zile wanazokuwa wanazifanya bila ya kutazama changamoto zinazowakabili, shauku inaanza kwa kuipenda kwanza kazi yoyote ile ambayo unaifanya kwani kwa kufanya hivyo kunaleta ufanisi katika kazi, kadhalika amesema kuwa kuna faida kubwa ya kuiwazia mazuri kazi yako na kuiga mfano wa watumishi wengine waliofanikiwa katika kazi zao hii itaongeza ufanisi na kuongeza shauku ya kazi.
Aidha Mwanasheria Method amewataka Watumishi wa Umma kuwa waadilifu, kuacha kujiingiza katika kashfa zozote mbaya kwa kutumia cheo au nyadhifa ya serikali vibaya kuwatapeli, kuwazurumu au kuwanyanyasa wananchi kwa namna yoyote ile kwa kigezo cha cheo au nyadhifa uliyonayo kama Mtumishi wa Umma.
"Tuwe waaminifu, tusiwe waongo, tunapokuwa waaminifu, wawazi bila ya kuficha jambo au kitu basi tunajenga imani nzuri kwa wananchi wanatuamini, unamkuta Mtumishi anaenda kulewa pombe za watu halafu halipi wakimuuliza anasema yeye ni Mtumishi wa Umma hii haikubaliki Watumishi Wenzangu".
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa