Mwenge wa Uhuru ulipokelewa Mkoani Iringa katika Wilaya ya Mufindi Kata ya Mapanda tarehe 02/09/2022, na hatimaye kuipokelew katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa shangwe kubwa sana.
Pamoja na mapokezi hayo Mwenge wa Uhuru umeweza kupitia miradi mbalimbali ikiwemo kuzindua Klabu ya Kudhibiti na Kupambana na madawa ya kulevya katika Shule ya Sekondari Ilambilole. Klabu ilianzishwa tarehe 30.02.2022 ikiwa na wanachama 15, ikitumika kama jukwaa linalowaleta pamoja wanafunzi ili kuibua mijadala inayohusu dawa za kulevya na jinsi zinavyoathiri juhudi za Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kukuza uchumi.
Mradi wa Pili ambapo Mwenge wa Uhuru ulipitia ni kukagua na kuzindua Kituo cha Afya Kiwele, ambapo Mradi huu umepokea fedha jumla ya Tsh 500,000,000 fedha za Serikali ambazo kwa awamu ya kwanza tulipokea kias cha Tsh 250,000,000 zikiwa na malengo ya ujenzi wa jengo la kutolea huduma kwa wangonjwa wa nje (OPD), jengo la maabara, choo matundu 6 na kichomea taka. Awamu ya pili tulipokea kiasi cha Tsh. 250,000,000 zikiwa na lengo la kujenga jengo la Wodi ya wazazi, jengo la upasuaji, jengo la kufulia na njia za kutembea kwa miguu (walk ways).
Utekelezaji wa mradi huu ulianza tarehe 1/03/2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 2/11/2022. Ujenzi wa mradi huu unatumia njia ya ‘’force akaunti’’ kwa kufuata muongozo uliotolewa na mamlaka ya udhibiti wa ununuzi ya umma PPRA wa mwezi Mei mwaka 2020.
Katika mradi wa Tatu Mwenge wa Uhuru umeweza kuzindua Klabu ya Wanafunzi ya mapambano Dhidi ya Rushwa katika shule ya Sekondari Kalenga na Ujenzi wa vyumba vine vya Madarasa na Ofisi mbili (MRADI NA.5441 TCRP). Ujenzi huu umetumia Jumla ya kiasi cha Tsh.92,646,450/= ambapo fedha kutoka Serikalini ni Tsh. 80,000,000/= na Mapato ya Ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni 12,646,450/=. Ujenzi umekamilka kwa 100%.
Mradi wa Nne ambao ulitembelewa na Mwenge wa Uhuru ni Daraja la Tosamaganga ambapo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetekeleza mradi wa ujenzi wa daraja la Tosamaganga lenye urefu wa Mita 20 kwa kutumia fedha za Maendeleo kutoka Mfuko wa Barabara. Daraja hili limejengwa kutokana na daraja lililokuwepo ambalo lilikuwa ni daraja la mbao lenye njia moja kuchakaa na kuweza kusababisha ajali na watu wanaopita kwa miguu kutokuwa na usalama.
Gharama za ujenzi wa daraja hili ni jumla ya cha TZS. 1,538,000,000.00 zilitengwa katika kutekeleza Mradi huu wa daraja, ikiwa ni TZS 890,000,000.00 na TZS. 700,000,000.00 katika mwaka wa fedha 2017/2018 na 2020/2021. Jumla ya TZS. 1,405,052,958.44 zimekwisha tumika katika utekelezaji na Mradi umekamilika na unatumika.
Mradi wa Tano Mwenge wa Uhuru uliweza kutembelea ni Bwawa la Maji katika Kata ya Masaka. Bwawa linalojengwa katika Kata ya Masaka, yenye vijiji vitatu; Sadani, Makota na Kaning’ombe, ambavyo kwa muda mrefu havina maji ya uhakika. Bwawa hili linajengwa na Wizara ya Maji kupitia ya Bodi ya Maji Bonde la Rufiji, kwa ajili ya kuvuna Maji ya Mvua ili kuongeza upatikanaji wa rasilimali za maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya nyumbani, mifugo, Kilimo cha umwagiliaji, na uvuvi.
Ujenzi wa Bwawa la Maji Masaka umefadiliwa na Serikali ya Tanzania, kupitia Wizara ya Maji chini ya Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa utaratibu wa “Force Account”. Jumla ya fedha kiasi cha Shs. 900,982,000 zitatumika kukamilisha ujenzi wa mradi. Mpaka sasa Jumla ya fedha Shs. 501,638,870 imeshatumika sawa na asilimia 55.67% ya fedha zote. Kwa ujumla Ujenzi wa mradi umeanza tarehe 20 Mei 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Octoba 2022.
Mradi wa Sita ambapo Mwenge wa Uhuru ulitembelea ni Kikundi cha Vijana cha Agri -Lishe kipo katika Kata ya Ifunda Kijiji cha Ifunda. Kikundi hiki kinajishughulisha na kuzalisha miche ya parachichi ya kisasa, kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kilimo cha parachichi kiuchumi, na kiafya, pia kufanya kliniki kwenye mashamba ya wateja na kutoa ushauri juu ya mbinu sahihi za utunzaji wa miche shambani. Kikundi kinatekeleza shughuli zake katika kijiji cha Ihemi.
Kikundi cha vijana Agri -lishe kilianzishwa mnamo tarehe 04/04/2021 na kusajiliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa namba. IDC/YEG/550. Kikundi kilianzishwa baada ya kuhamasishwa na Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata ya Ifunda. Kikundi kina jumla ya wanachama 5 kati yao Wanaume ni 3 na Wanawake ni 2.
Kikundi cha vijana Ari -lishe kimepata fursa mbalimbali tangu kuanzishwa kwake zikiwemo kuunganishwa na mamlaka ya uthibiti wa mbegu (TOSCI) na kupatiwa mafunzo yaliyolenga kujengea uwezo katika uendelezaji wa upandaji wa miche yenye ubora na kiwango kinachohitajika sokoni. Kikundi pia kimeunganishwa na Umoja wa wazalishaji wa parachichi Tanzania (ASTA) ili kupata taarifa za masoko mbalimbali na ubora na elimu juu ya ubora wa miti ya parachichi shambani. Kikundi kimeendelea kupata elimu ya uongozi na utunzaji wa kumbukumbu. Kikundi kimepata fursa ya mkopo wa fedha za asilimia nne (4%) sisizo na riba zinazotolewa na Halmashauri kiasi cha Tsh 10,000,000/=, ambayo iliwezesha kukamilisha mradi wa Kikundi cha Vijana Agri- Lishe. Pamoja na jitihada za nguvu za wanachama, kikundi kina fedha kiasi cha Tsh. 15,000,000/=, na Tsh. 10,000,0000/= kutoka Mkopo wa Halmashauri na kufanya jumla ya Tsh. 25,000,000/=
Mwenge wa Uhuru baada ya kukagua iliridhia kuwa miradi yote ni mizuri na ipo kwenye kiwango kinachotakiwa na ikazinduliwa. Hatimaye mkesha wa Mwenge wa Uhuru ulikesha katika Kata ya Ifunda Kijiji cha Ifunda.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa