Mh.Mhapa amuahidi Mkuu wa Mkoa ushirikiano kwa ajili ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mh.Stephen Mhapa amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa maneno mazuri ambayo yameonyesha matumaini na ushirikishwaji katika kuyapatia uvumbuzi kero za wananchi wa Halmashauri yake lakini pia kuongeza kazi ya maendeleo kwa wananchi.
“tunakushukuru sana Mkuu wetu wa Mkoa wa Iringa kwa kufungua milango na kuomba tukupe ushirikiano na sisi pia tunaomba ushirikiano wako ili sote kwa moja tushirikiane na kwa mwanzo huu tunaamini Mkoa wetu unaenda kubadilika sasa”Alisema.
Nanye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Bw.Bashir Muhoja amewatoa hofu Waheshimiwa Madiwani kuwa Serikali imeweka utaratibu mzuri wa matumizi ya fedha zinazokuja nje ya bajeti lakini pia ukingoni mwa mwaka wa fedha kuwa fedha hizo hazitarudiserikali kuuzitztumika kwa miradi iliyokusudiwa.
“Niwatoe hofu fedha zipo salama na hazitarudi serikali kuu kwa kushindwa kutumika zitatumika zote katika miadi iliyokusudiwa na miradi mingi imefanyika kwa kiwango cha juu na kuonyesha thamani ya fedha iliyotumika”alisema Bw.Muhoja.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa