Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi -CCM Mkoa wa Iringa asifu ubora na viwango katika miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa aliyoitembelea na kukagua.
Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa – DC)
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM Mkoa wa Iringa Mh.Abel Nyamhanga ameridhishwa na kazi na ubora wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuwa inaonyesha thamani ya pesa.
Mh.Nyamhanga ametoa kauli hiyo Julai 20,mwaka huu wakati akihitimisha ziara yake ya siku moja katika Halmashauri hiyo ambapo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na timu yake kwa kazi nzuri ya ufuatiliaji na usimamizi ambao ndio msingi wa kazi nzuri iliyofanywa katika miradi yote aliyopitia na kusema kuwa ubora huo unakipa heshima kubwa Chama Cha Mapinduzi ambacho kimeahidi katika ilani yake.
“Mh.Mwenyekiti wa Halmashauri,Mkurugenzi Mtendaji na timu yako nawapongeza sana sio rahisi kamati ya siasa kupongeza lakini nitakuwa wa ajabu kama sitalisema hili hap ana kusubiri kifo ndio niseme kuwa aliyesimamia ujenzi huu alifanya vizuri kwa niaba ya Kamati ya Siasa Mkoa tunawapongeza kwa dhati kwa usimamizi mzuri”alisema.
Katika ziara hiyo Mh.Nyamhanga alikagua mradi wa Daraja lililopo Kijiji cha Tosamanga,Bweni la Watoto wenye mahitaji maalum, Vikundi vilivyowezeshwa na asilimia 10 ya makusanyo ya mapato ya ndani,ujenzi wa kituo cha afya Migoli,Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na ujenzi wa wodi tatu katika hospitali ya Wilaya ya Iringa Igodikafu iliyopo Tarafa ya Pawaga Kijiji cha Mbuyuni.
Aidha akiwa katika ziara hiyo Mwenyekiti Nyamhana aliwapongeza Viongozi wa Halmashauri kwa kutekeleza vyema ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kwamba suala hili ni agizo la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa