JICA, FAO na RUDI wawekeza katika sekta ya kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano,Iringa- DC)
Kamati ya Uchumi,Ujenzi na Mazingira imefanya ziara ya kukagua mradi wa skimu ya umwagiliaji ya Mafuruto na ghala katika Skimu ya umwagiliaji ya Mlenge inayofadhiliwa na mashirika ya Kimatifa .
Akisoma taarifa ya miradi hiyo Kaimu Afisa Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika Bi.Clementina Kabaka ameeleza kuwa mradi wa skimu ya umwagiliaji Mafuruto umefadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na mradi wa ghala la skimu ya umwagiliaji ya Mlenge unafanywa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Taasisi ya RUDI kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya yaa Iringa.
Bi.Kabaka amefafanua gharama za miradi hiyo kuwa ni Skimu ya umwagiliaji ya mafuruto imeghaIimu kiasi cha shilingi milioni 400,965,800/= na ghala la skimu ya umwagiliaji Mlenge ambalo ujenzi bado unaendelea limetegewa kiasi cha 437,005,858.75/= ambapo mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa jumla ya shilingi 219,747,252.68/=.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Ponsiano Kayage amepongeza kazi nzuri iliyofanyika katika miradi hiyo lakini pia ameipongeza serikali kwa ushirikiano mzuri wa kimataifa unaopelekea nchi rafiki kusaidia katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.
“Naipongeza sana serikali yetu kwa mahusiano mazuri na nchi mbalimbali duniani hali iliyopelekea mashirika ya JICA,FAO na Taasisi ya RUDI kutusaidia katika masuala ya maendeleo katika Halmashauri yetu ya Wilaya ya Iringa” na kuongeza kuwa
“Tija itaongezeka sana kwa wakulima wetu kwani sehemu ya uhakika ya kuhifadhia mpunga itakuwepo tena karibu na makazi yao,niombe kwa viongozi uwepo wa ghala hili hapa ni fedha ambazo serikali imeweka litumike kwa lengo lillokusudiwa”amesema.
Aidha,Mh. Kayage alitoa shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa uhodari wake katika usimamizi wa shughuli za Maendeleo pamoja na Wataalam wa Halmashauri ambao wamekuwa wasikivu mara zote kwa kupokea mawazo na kuyafanyia kazi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa