NAIBU WAZIRI DUGANGE AFURAHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LA NGANO – IGULA IRINGA DC
Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI (Afya) Mhe. Dkt. Festo Dugange amefurahishwa na kupongeza kazi ya ujenzi wa daraja la Ngano – Igula lililojengwa kwa mawe alipotembelea eneo hilo 19.12.2023.
Daraja hilo linalounganisha vijiji mbalimbali vya Tarafa ya Isimani na hata Wilaya ya Kilolo lina urefu wa km 34 na limegharimu kiasi cha shilingi milioni 225 gharama ambayo ni nafuu ukilinganisha na kama lingejengwa kwa utaratibu wa kawaida ambapo lingegharimu Zaidi ya shilingi Bilioni 2.
Mhe. Dkt. Dugange ametoa wito kwa wahandisi wa Wilaya na Mikoa mingine kufika na kujifunza teknolojia hii rahisi inayotumia malighali inayopatikana kwenye maeneo husika ambayo ni mawe ili kuweza kuitumia kwenye maeneo mengine.
“Nitumie nafasi hii kuwapongeza sana wananchi wa vijiji hivi na Wilaya hii kwa ujumla kwa zawadi kubwa hii mliyoipata ya daraja ambalo ni mkombozi kwa shughuli zetu za kila siku, shughuli za kijamii na kiuchumi. Lakini pia daraja hili limegharimu kiasi cha takribani shilingi milioni 225, lina urefu wa mita 34 limetumia madini ya asili yanayopatikana kwenye maeneo yetu… na kuokoa Zaidi ya Bilioni 1 na milioni 800”
Aidha Mhe. Dkt. Dugange amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa Kuongeza bajeti ya TARURA mara dufu iliyowezesha kuboreshwa kwa mitandao ya barabara.
Mhe. Dkt Dugange pia alitembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha Afya Malengamakali pamoja Shule ya Sekondari William Lukuvi na kuagiza kuwa mapungufu yaliyojitokeza yafanyiwe kazi ili kazi iliyokusudiwa ikamilike kwa wakati na huduma iendelee kutolewa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa