NAIBU WAZIRI WA ARDHI AWAAGIZA WAKURUGENZI KUWASIMAMIA MAAFISA ARDHI KATIKA MAENEO YAO.
Na Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano, Iringa –DC)
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba, na Maendeleo ya Makazi ,Mh Angeline Mabula amewataka Wakurugenzi kuwasimamia na kufuatilia utendaji wa kazi wa Maafisa Ardhi kwa kuwa kiutendaji bado wapo katika Mamlaka zao.
Mh Mabula alisema hayo Mei 16 mwaka huu alipokuwa katika ziara yake Mkoani Iringa ambapo alikagua Masijala ya Ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kuagiza wadaiwa sugu wote wafuatiliwe ili walipe madeni yao ndani ya siku kumi na nne iwapo hawatatekeleza wapelekwe katika baraza la Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa hatua zaidi za kisheria.
“Huu sio muda wa kubembelezana waandikieni hati za kuwakumbusha kulipa ni vizuri kwa kuwa sio wote wenye nia ovu ya kukwepa kulipa kodi, na nasheria humtaka alipie ndani ya siku kumi na nne kushindwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria hivyo naagiza wapelekwe katika Baraza”alisema.
Pia, Mh Mabula alisisitiza utolewaji wa hati kwa wananchi uwe wa haraka, kwani hiyo ndio sababu ya kuanzishwa kwa Ofisi za Mikoa za Ardhi, na wananchi wanufaike na hati hizo na sio vinginevyo.
“Lengo la kuanzishwa Ofisi za Mikoa za Ardhi ni kurahisisha upatikanaji wa hati kwa wananchi wote wlionunua ardhi ili ziweze kuwasidia katika masuala mbalimbali ya kiuchumi,kwa kuwa huzitumia hati hizo kama sehemu ya dhamana wanapokuwa wanaomba mikopo katika taasisi za fedha”na kuongeza
“Naagiza utaratibu mzuri wa utunzaji wa kumbukumbu za Ardhi uzingtiwe ili kusiwe na usumbufu kwa wananchi wanapokuwa wanafuatilia Hati zao,lengo la Serikali ni kuondoa kero sio kuzalisha kero”alisema.
Aidha Naibu Waziri huyo aliangiza kufanya vipindi maalum vya redio kuhamasisha wananchikulipa kodi hizo au kutumia mfumo wa kutangazia Umma kwa njia ya vipaza sauti.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa