NBS Yatoa Mafunzo ya Matokeo ya Sensa ya 2022
“Napenda kuwakumbusha kuwa, madhumuni ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 ni kukusanya taarifa za kidemografia, ikuchumi, kijamii na mazingira ya watu wote walioko nchini kwa mtawanyiko wake ili kusaidia katika kupanga, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa sera, mipango na program za maendeleo ya nchi”.
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Wilaya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy, alipokuwa anafungua mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yaliyofanyika Oktoba 06, 2023 katika Ukumbi wa Masiti Grand.
Ameongeza kusema kuw, mafunzo hayo ya matumizi ya matokeo ya Sensa kwa makndi mbalimbali katika jamii yetu yanayoendeshwa na Ofisi ya Taifa ya Takwemu na Ofisi ya Mtakwemu Mkuu wa Serikali Zanzibar, kwani ni sehemu ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Usambazaji na mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya mwaka 2022.
Aidha, Mheshimia Kessy amesisitiza umuhimu wa mafunzohaya ya kwa washiriki na kuwahikikishi kuwa, huu ni mwanzo wa mfululizo wa mafunzo kama haya kwa Viongozi na Watendaji wa Serikali.
Naye Mtakwimu Mkoa wa Iringa Ndugu Peter Millinga, amewashukuru washiriki kwa kuhudhuria mafunzo hayo kwa wingi na kwa usikivu na umakini mkubwa.
Mwisho wa mafunzo NBS walitoa ramani ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kupokelewa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Steven Mhapa, ikifuatiwa ramani ya kila Kata ambazo zilipokelewa na kila Diwani husika wa Kata.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa