Nishati Safi ya Kupikia Kwa Wote!
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimwa Halima Dendengo, leo ameendelea kuongoza Mjadala wa Kitaifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa upande wa Mkoa wa Iringa. Mjadala huu ulianza jana Novemba 1, 2022 na umemalizika leo Novemba 2, 2022.
Akizungumza wakati akichangia hoja kwenye mjadala huo ambao umeendeshwa kwa njia ya mtandao, Mheshimiwa Dendego amesema, “suala la nishati na umuhimu wake lilichukuliwa kwa uchache sana na baadhi ya watu na kudhani nishati ya kuni na mkaa ni kwa ajili ya wananchi wa hali ya chini tu, kumbe nishati safi inapaswa kutumika kwa kila mwananchi bila kujali hali yake ya kimaisha au kiuchumi.”
Mheshimiwa Dendego ameendelea kusema kuwa, “nchi ya Tanzania ina vyanzo vingi vya nishati, kwa hiyo Wadau waiangalie Tanzania na kuboresha miundombinu yake na hatimaye iweze kutoa nishati safi ambayo itatosheleza mahitaji ya kwa kila Mtanzani. Pia elimu itolewe kwa wananchi ili kila mtu awe na uelewa juu ya jambo hili”.
Mheshimiwa Dendego amemaliza kwa kusema kuwa, “tunamhakikishia Waziri wa Nishati Mheshimiwa Januari Makamba kuwa, sisi wana Iringa tupo tayari kwa mabadiliko, na tunaahidi tutakuwa vinara wa nishati safi”.
Mjadala umeendelea kwa wajumbe na Wadau kwa kuchangiabmada mbalimbali ambazo ziliwasilishwa. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais, kikosi kazi kihusishe Sekta Binafsi, ili kuweka mkakati wa pamoja katika kufanikisha jambo hili.
Mkutano huu umefanyika Mubashara kutoka Jijini Dar es Salaam na kuunganishwa kwa Mikoa ya Iringa, Tabora, Shinyanga na Morogoro.
Akifunga mjadala huo Waziri wa Nishati Mheshimiwa Januari Makamba amesema, “tumefanikiwa sana zaidi ya tulivyotarajia katika mjadala huu, hasa tulipotoa mwaliko kwa Mama zangu Prof. Anna Tibaijuka, Dkt. Getrude Mongela na Dkt. Zackia Meghji kwa kukubali mwaliko huu”
Mheshimiwa Mkamba ameendelea kusema kuwa, “Mnatupongeza sisi kwa kuandaa mjadala huu, lakini sisi tunawashukuru ninyi kwa kuja na kushiriki. Tumepata hamasa kubwa kwa maneno ya Mheshimiwa Rais, kwa kututia moyo juu ya jambo hili. Hivyo tunaenda kujipanga na kujidhatiti kufanikisha jambo hili”
#nishatisafiyakupikia
#ortamisemi
#msemajimkuuwaserikali
#ikulu
#januarimakamba
#rsiringa
#halimadendego
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa