Kipindi cha “Nyota ya Asubuhi” Chaing’arisha Iringa DC
“Tatizo la vyoo bora na vya kisasa limemalizika katika Shule za Msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Iringa”…Kauli hii imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja alipokuwa katika kipindi cha Nyota ya Asubuhi kinachorushwa na Radio Furaha Fm, ambayo inapatika Manispaa ya Iringa leo Septemba 20, 2023.
Wakili Muhoja alikuwepo kwenye kipindi hicho akizungumzia mambo mbalimbali yanayohusu Halmashauri hiyo, na kwamba anajivunia sana kuondoa tatizo la vyoo kwa shule za msingi. Hata hivyo majengo ya madarasa ya shule za msingi na sekondari na uanzishwaji wa shule mpya 4 za sekondari ambazo zimejengwa katika Kata nne za Halmashauri ambazo ni Kata ya Luhota, Kata ya Mlenge, Kata ya Ulanda na Kata ya Mboliboli zitakazoondoa msongamano wa wanafunzi katika shule za jirani na kutembea umbali mrefu kwa watoto kufuata elimu. Hii imetokana na muamko mkubwa kwa wananchi kwa uelewa wa kuwapeleka watoto shule, na ufaulu mzuri unaopatikana katika Halmashauri kwani haijawahi kushuka chini ya 92% kwa ufaulu.
Aidha katika kipindi hicho Wakili Muhoja ameishukuru Serikali kwa kutoa pesa kiasi cha Shilingi Bilioni 3 ambazo zilitolewa kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Utawala za Halmashauri zilizojengwa katika Kijiji cha Ihemi Kata ya Mgama ambapo huduma zote muhimu zinapatikana hapo.
Pamoja na mambo mengine Wakili Muhoja ameweza kugusia miundombinu ya barabara, ajira kwa Kada mbalimbali, mazingira na hali ya uchumu na mapato kwa Halmashauri.
Muhoja ameendelea kusema kuwa, “pamoja na mafanikio hayo yote, Halmashauri bado inapungukiwa na watumishi hasa katika Kada ya Walimu na Afya, nina Imani na Serikali itaendelea kutoa ajira na kuwakaribisha ambao wapo tayari kujitolea kwa ajili ya kujenga Halmashauri yetu, na mwisho wa siku wanaweza kupata ajira ya kudumu”.
Pia changamoto za tabianchi anasema ni mojawapo inayosababisha ukosefu wa mapato hasa katika Bwawa la Mtera. Kupungua kwa maji na kusababisha samaki kupotea na kufanya wavuvi wasiweze kufanya shughuli zao zinazowaingizia kipato.
Kadhalika Wakili Muhoja anawakaribisha Wadau mbalimbali kuja kuwekeza Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwani kuna fursa mbalimbali kama viwanja vya makazi, viwanja vya kwa ajili ya viwanda, shughuli za uvuvi, kilimo na nyingine nyingi.
Baadhi ya wananchi waliweza kutoa maoni yao na kuuliza maswali mbalimbali, Wakili Muhoja ameweza kuzichukua na kwenda kuzifanyia kazi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa