• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe Za Watumishi |
Iringa District Council
Iringa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu sekondari
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Mazingira na Usafishaji
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA NA Uhusiano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango,Utawala na Uchumi
      • UKIMWI
      • Afya Elimu na Maji
      • UMazingira, uchumi na Ujenzi
      • Maadili
    • Ratiba Ya Vikao mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Hudumakwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video za Shughuli Mbalimbali za kiofisi na za Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

PELEKENI TABASAMU KWA WANANCHI KIUTENDAJI - PROF. SHEMDOE

Imewekwa : November 19th, 2025

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewataka watumishi na viongozi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa upendo, amani na mshikamano ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa ubora na kuachiwa tabasamu kupitia huduma zinazotekelezwa na Serikali.

Akizungumza mara baada ya kupokelewa na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI katika makao makuu ya wizara hiyo Mtumba nje kidogo ya Jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuwaachia Watanzania tabasamu ifikapo mwaka 2030, na kusisitiza kuwa TAMISEMI ina jukumu la moja kwa moja katika kutimiza azma hiyo.

Amesema watumishi wanapotekeleza majukumu yao katika ngazi ya mikoa, wilaya, halmashauri, kata, vijiji, mitaa na vitongoji wanapaswa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zinazoendana na mahitaji yao na kuwapa tabasamu linalotarajiwa kwa wananchi linapaswa kuanzia kwa watumishi wenyewe kupitia utendaji uliokamilika na wa kuheshimu utu.

Aidha, Prof. Shemdoe amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kuongoza wizara hiyo, pamoja na wananchi wa Lushoto waliompa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia kama Mbunge wa Jimbo hilo.

Kwa upande wa Naibu Waziri anayeshughulikia Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI Mhe.Reuben Kwagilwa amesema wizara itaendelea kuongeza ushirikiano na ufanisi ili kuhakikisha sekta hiyo inatoa huduma bora zinazochochea maendeleo na kuongeza tabasamu kwa wananchi.

Naye Naibu Waziri anayeshughulikia masuala ya Afya OWM-TAMISEMI, Mhe.Dkt. Jafar Seif, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na ushirikiano ili kuboresha huduma za Afya hususan katika ngazi ya Afyamsingi ambazo zinawagusa wananchi moja kwa moja.

Mapema leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka mawaziri wote wateule kutekeleza kwa kasi ahadi 100 za Serikali ya Awamu ya Sita ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma za uhakika na kwa wakati.

Wizara ya TAMISEMI imeahidi kuendelea kuimarisha utendaji na kuwasogezea wananchi huduma bora zitakazowafanya waishi kwa matumaini na tabasamu.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI JIMBO LA KALENGA & ISMAN October 12, 2025
  • Happy Nyerere day October 14, 2025
  • KUITWA KWENYE USAHILI WA UBORESHAJI WA DAFTARI JIMBO LA KALENGA NA ISMANI December 06, 2024
  • FURSA YA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) January 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TUKAWE MABALOZI WAZURI KWENYE JAMII ZETU KUTOKOMEZA UKATILI - NDG MASUNYA

    November 21, 2025
  • PELEKENI TABASAMU KWA WANANCHI KIUTENDAJI - PROF. SHEMDOE

    November 19, 2025
  • DED IRINGA DC AFUNGUA KIKAO KAZI CHA UANDAAJI WA MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI

    November 12, 2025
  • MKURUGENZI IRINGA DC AKABIDHI GARI MPYA KWA AJILI YA SHUGHULI ZA AFYA NA USAFI WA MAZINGIRA

    October 20, 2025
  • Tazama zote

Video

Makala kuhusu miundombinu ya elimu
video

Viungo vya haraka

  • FOMU YA USAJILI WA VIKUNDI
  • INGIA KWENYE MFUMO WA VIKUNDI VYA HUDUMA NDOGO ZA FEDHA
  • Salary slip

Viungo vinavyohusiana

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais-Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora
  • Sekretariati ya ajira
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti kuu ya takwimu huria
  • Tovuti Rasmi ya Rais

Idadi ya watembeleaji duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

https://bachelorthesiswritingservice.com

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Kijiji cha Ihemi

    Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa

    Simu ya mezani: 026-2702828/2702585

    Simu ya mkononi: 0757 364 994

    Barua pepe: ded@iringadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa