Ummi Mohamed (Afisa Habari na Uhusiano, Iringa -DC )
Watumishi wakumbushwa umuhimu wa kujikinga na vitendo vinavyikinzana na Maadili ya Utumishi wa Umma.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wameendelea kukumbushwa maadili ya Utumishi wa Umma ikiwemo kutojihusisha na vitendo vyovyote vya rushwa ikiwemo rushwa ya ngono.
Mkurugenzi Mtendaji aliwataka watumishi kuendelea kutekeleza wajibu wao kuwahudumia wananchi katika maeneo yao ya kazi ili kutimiza lengo la Serikali la kuhakikisha huduma zote muhimu zinawafikia wananchi waliopo chini.
Naye, Afisa Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa Bw.Ditram Muhoma Akitoa mada ya Utawala Bora amesema ni budi kutojihusisha na rushwa za aina zote kwa kuwa makosa yote ya rushwa sasa yanahesabiwa kama makosa ya kuhujumu Uchumi.
Bw.Muhoma amesema kukumbushana ni suala la msingi katika uboreshaji wa utendaji kazi kwa weledi ili kuepuka kuingia ama kutenda makosa ambayo sio ya lazima na yanaepukika katika maeneo ya kazi.
Aidha akitoa mada kuhusu uhusiano wa ugonjwa wa Ukimwi na Kifua Kikuu kwa niaba ya Mganga Mfawidhi Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya Iringa Dkt. William Mbuta amesema mgonjwa wa Kifua Kikuu akitumia dawa kwa usahihi na kufuata masharti ya utumuaji wa dawa na lishe anapona kabisa ugonjwa huo,
Dkt.Mbuta amesema ugonjwa wa Kifua Kikuu unauhusiano na ugonjwa wa Ukimwi kwa kuwa vipimo vimekuwa vikionyesha asilimia kubwa ya watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi pia wanaugua Ugonjwa huo wa Kifua Kikuu.
Pia,ametoa rai wa watumishi wote kujikinga na maambukizi ya Maradhi haya ikiwa pamoja na kutoa elimu katika jamii wanamoishi ya matumizi sahihi ya mipira kinga ya kike na kiume (kondomu) ili kuwezesha kupungua kwa maambukizi mapya ya Ugonjwa huo.
Wakihitisha kikao hiko Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Utumishi Mkuu wamewakumbusha Watumishi juu ya suala zima la uwajibikaji katika maeneo yao na kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa