RAIS SAMIA ATOA ZAWADI YA KRISMASI KWA WATOTO YATIMA IRINGA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya Sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwa ni pamoja na vitoweo ,mchele , maharage,mafuta ya kupikia, sabuni, chumvi na viungo vingine mbalimbali vya kupikia.
Akimuwakilisha Rais kukabidhi bidhaa hizo katika kituo cha kulelea watoto yatima Tosamaganga kilichopo Kijiji cha Tosamaganga Kata ya Kalenga Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Halima Dendego amesema kituo hicho kimeviwakilisha vituo vingine.
Ameeleza kuwa Rais kwa kutambua makundi maalum ametoa zawadi hizo ili watoto hao washeherekee kama watakavyosheherekea watoto wengine majumbani hivyo amesema kupitia majitoleo hayo watakuwa wameuona mkono wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Nimekuja hapa leo na salamu za upendo kutoka kwa Mh. Rais wetu, kwa kutambua jukumu kubwa mlilonalo la kulea hawa watoto, na yeye amewiwa kuchangia katika sherehe hizi za kuzaliwa Kristu, ameniagiza nilete zawadi kutoka kwake kwa ajili ya watoto hawa ili na hawa watoto wajione kama wako nyumbani na mama na baba.β
amewaletea zawadi pamoja na salamu za Sikukuu za Krismasi, ambapo amewaletea Mbuzi wanne, Mchele, Maharage, Mafuta, na Viungo vingine mbalimbali. amesema Dendego.
Aidha Mhe. Dendego kwa niaba ya watoto na wananchi wa Mkoa wa Iringa amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watoto hao.
βna sisi pia tunakutakia Krismasi njema, Afya njema kazi kubwa unayoifanya Mheshimiwa, Mwenyezi Mungu azidi kukusimamia na kukuongoza, Tunakushukuru kwa zawadi hii ulioileta Iringa kwa ajili ya watoto wetu tunasema asante sana.β
Naye Kiongozi wa Malezi ya Watoto Tosamaganga Sista Hellena kwa niaba ya Watoto, Masista na wafanyakazi amemshukuru Mhe Rais na Mkuu wa Mkoa kwa zawadi hizo za Krismasi.
Kituo cha kulea watoto cha Tosamaganga kina jumla ya watoto mia mbili na wana watoto kuanzia umri wa miezi miwili na kwa sasa kuna jumla ya watoto 72 ambao bado ni wadogo hawajaanza shule na wengine wametawanyika katika shule mbalimbali wakipata elimu.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa