Ahimiza umakini, ubunifu, kutoa taarifa sahihi na matumizi ya teknolojia katika kuuhabarisha ummma.
Katibu Tawala ya Mkoa wa Iringa Bi. Doris Kalasa amefungua kikao kazi cha maafisa Habari wa Mkoa wa Iringa kilichofanyika katika Ukumbi wa Katibu Tawala wa Mkoa Februari 05, 2025.
Akizungumza na maafisa Habari Bi. Kalasa ametoa msisitizo kwa maafisa Habari kuwa makini, wabunifu na kutoa Habari zilizo sahihi ili kulinda dhamira ya serikali na kuhakikisha wananchi wanapata Habari za kweli na kwa wakati.
Aidha Bi kalasa amezungumzia uwajibikaji katika kuuhabarisha umma, “Maafisa Habari mna nafasi kubwa katika kuimarisha uhusiano wa serikali na wananchi, wananchi wanahitaji kuaminishwa kuwa serikali yao inafanya kazi kwaajili yao na hii inawezekana tu kupitia taarifa sahihi za wazi na zenye manufaa kwao”
Kwa upande wao maafisa Habari wamekiri kupokea maelekezo na nasaha kutoka kwa katibu tawala wa mkoa na kuahidi kuyafayia kazi sanjari na mjadala wa ajenda ambazo zimepangwa kujadiliwa.
Kikao hiki kimehusisha maafisa Habari kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kikiwa na lengo la kuboresha utendaji kazi wa maafisa Habari katika utekelezaji wa majukumu yao, usimamizi wa mawasiliano ya umma, uimarishaji wa mifumo ya utoaji taarifa na kujenga uwezo katika masuala ya Habari na mawasiliano ya serikali.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa