RC Dendego Alia na Mamba Mtera
Matukio ya watu (wavuvi) kuliwa na mamba katika Bwawa la Mtera lililopo Kata ya Migoli, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendego amefanya ziara kwenye Kata hiyo na kuweza kuongea na wananchi wanaovua katika bwawa hilo Januari 10, 2024.
Mheshimiwa Dendego amesikiliza maoni yao na kutaka kufahamu nini kifanyike ili kukabiliana na mamba hao, ambapo wananchi hao wamemuomba kutumia silaha za asili kama ndoano ili kuwanasa mamba hao, kwani silaha kama bunduki zimeshindwa kufanya kazi majini.
Akipokea maoni ya wananchi hao Mheshimiwa Dendego ametoa maagizo kwa viongozi wa maeneo hayo kuwataka kuanza kazi mara moja ya kutega ndoani hizo kwa kushirikiana na Taasisi ya TAWA ambayo inahusika na wanyama pori.
Aidha mheshimiwa Dendego ametoa maagizo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kufanya tathmini ya vikundi vya wavuvi na idadi ya wavuvi kwa ujumla, ili kuweza kuwasaidia kupata mkopo wa ununuzi wa boti ambazo watatumia katika shughuli za uvuvi, na kwamba mwaka wa Fedha 2024/2025 Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa boti na kusaidia kuondokana na changamoto ya mvuvi mmoja mmoja inayosababisha kuliwa na mamba kila wakati.
Wakati huo huo, Mheshimiwa Dendego ameweza kutembelea Shule ya Msingi Mtera na kujionea uandikishaji wa wanafunzi wa Awali na Darasa la Kwanza kwa mwaka 2024. Pia kuona uelewa wa wanafunzi kwa jinsi wanavyofundishwa darasani, na kwamba ameridhishwa na kazi zinazofanywa na Walimu hao.
Aidha, Mheshimiwa Dendego alifika hadi Shule ya Sekondari Nyerere, kujionea wanafunzi walioripoti wa Kidato cha Kwanza. Idadi ya wanafunzi walioripoti shuleni hapo ni 32 tu na kuona idadi ni ndogo ikilinganishwa na wanafunzi 386 waliopangwa kuanza Kidato cha Kwanza shuleni hapo hivyo hakuridhishwa na jambo hilo.
Mheshimiwa Dendego ametoa maagizo kwa Mtendaji wa Kata hiyo ya Migoli kwa kumuambia kuwa, kwa kushirikiana na viongozi wa Kata hiyo na akiwemo Diwani, kupita nyumba kwa nyumba katika kila Kijiji kukagua ni mzazi gani ambaye hajampeleka mtoto kwenda kuanza shule na kuripoti Kidato cha Kwanza.
Mheshimiwa Dendego ameendelea na ziara yake hadi Kata ya Kising’a na kukagua Zahanati iliyopo Kijiji cha Matembo. Zahanati hiyo ilijengwa kwa msaada wa Mdau Ndugu Asas Abri, kwa gharama ya Shilingi Milioni 180. Mheshimiwa Dendego na wananchi wa eneo hio wamemshukuru Mdau huyo kwa kuwasogezea huduma za afya karibu kwani walikuwa wanatembea umbali mrefu sana kufuata huduma hiyo. Zahanti hiyo imekamilika na imeanza kutoa huduma.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa