Tahadhari za Kiusalama Katika Kipindi Hiki cha Mvua Haarishi Ziwe
“Kipindi hiki tumeambiwa kutakuwa na mvua nyingi, lakini Mkoa wa Iringa haukuwepo kwenye orodha ya hali ya hatari kutokana na mvua hizi. Hivyo tunakumbushwa kuwa, tuchukue tahadhari za kiusalama kila inapotokea dalili ya mvua”.
Kauli hii imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Dendengo akiwa ameongozana na Kamati ya Ulinza na Usalama ya Mkoa alipokwenda kuwapa pole wananchi wahanga wa mafuriko katika Kata ya Migoli Desemba 08, 2023.
Ameongeza kusema kuwa, “pamoja na yote tumekuja kuwapa pole na kuwatia moyo wahanga wa mafuriko haya.”
Mheshimiwa Dendego ameaagiza Wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Iringa (TANROADS) kuwa, waje wafanye tathmini katika daraja lililokuwa limeziba na kusababisha uharibifu huo kutokana na maji yanayopita katika daraja hilo kuacha njia yake na kuingia majumbani, ili waweze kulifanyia marekebisho.
Mheshimiwa Dendego amewashukuru Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Veronica Kessy na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wakili Bashir Muhoja kwa kufanya jitihada za haraka kwa kwenda kuwanusuru wahanga hao kwa kuwapatia chakula.
Pole iliyotolewa na Mheshimiwa Dendengo ni pamoja na unga kilo 150, Mchale kilo 625, Mfuta ya kupikia Lita40, maharage kilo 160 na chumvi pakti 100.
Wakati huohuo Mheshimiwa Dendego aliweza kwenda kutoa pole kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Chapuya wa Kijijji cha Makatapole Kata ya Migoli, ambaye alikamatwa na mamba katika Bwawa la Mtera alipokuwa anafanya shughuli zake za uvuvi, na kwamba amepoteza maisha katika ajili hiyo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa