Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amehimiza usimamizi madhubuti wa miradi ya maendeleo ambayo fedha imeshatolewa Iringa dc, akisisitiza kuwa wakandarasi na mafundi wanaolipwa fedha za umma lazima wafanye kazi kwa viwango stahiki.
Mhe. Kheri amezungumza hayo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo Septemba 30, 2025 ikiwemo ujezi wa ujenzi wa Zahanati wenye thamani ya shilingi milioni 60 katika Kijiji cha Mlanda, Kata ya Magulilwa, Tarafa ya Mlolo, kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Lyandembela jata ya Ifunda na ujenzi wa vyumba vya maabara shele ya sekondari Lukuvi - Mapogolo kata ya Idodi.
Ziara hiyo ni sehemu ya mikakati ya ufuatiliaji wa karibu wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayofanywa na serikali ili kuhakikisha huduma za kijamii kama afya, elimu, na maji zinaboreshwa kwa kiwango kinachostahili.
#iringaimaratutaijengakwaumojanauwajibikaji
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa