RC IRINGA APOKEA VIFAA VYA UJENZI KUTOKA BENKI YA NMB
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amepokea vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na benki ya NMB kama sehemu ya kuimarisha uhusiano wa na jamii inayowazunguka.
Vifaa vilivyotolewa na wadau wa benki ya NMB ni kama ifuatavyo;
Hivyo kufanya jumla ya vifaa vilivyotolewa ni bati 900, misumari kg 700, mbao 1,500
Mhe. Dendego amepongeza wadau wanaoshirikiana na serikali katika kuchangia maendeleo na kusema kuwa, serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya na inaendelea kufanya mambo makubwa ya kuwaletea wananchi maendeleo, na kwamba mtu yeyote hapaswi kubeza kwani yanayofanywa yanaonekana wazi.
Pia Mhe. Dendego amempongeza Mbunge wa Jimbo la Isimani Mhe. William Lukuvi kwa kuwatafuta wadau wa benki ya NMB kuweza kuchangia vifaa vya ujenzi kwenye shule mbalimbali za eneo hilo.
Sanjari na hayo, Mhe. Halima Dendego ametambua changamoto ya kijiografia ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na kuona kuwa kuna uhitaji wa kuwa na halmashauri mbili. Hivyo ameelekeza kuwa taratibu za kupata Halmashauri mbili zianze na inapokuja RCC makubaliano yafikiwe na ombi lipelekwe ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Naye mbunge wa jimbo la Isimani Mhe. William Lukuvi ameshukuru na kufikisha salamu za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha za ujenzi wa Zahanati ya Magombwe milioni 120, na fedha za ujenzi wa nyumba ya mganga shilingi milioni 25, na fedha zingine zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Isele Kata ya Mlenge kiasi cha shilingi 339 kupitia mradi wa TASAF.
Pia Mhe. Rais ameamua kuifungua Pawaga ambapo kuna barabara ya lami itajengwa kuanzia Pawaga sekondari hadi Izazi na Itunundu kwenda Iringa mjini kuanzia mwaka 2024 na barabara zote hizi zitaanza kwa pamoja, amesema Mhe. Lukuvi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa