Ahimiza wasimamizi wa miradi kujiwekea mpango wa muda (deadline) ili kutoa nafasi kwa miradi mingine kuanza.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amepongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Mhe Serukamba ametoa pongezi hizo alipokuwa kweye ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika Januari 27 – 28, 2025 katika Jimbo la kalenga na Ismani.
“Kwanza kabisa niwapongeze kwa kasi ya ujenzi wa miradi inavyokwenda, ukiangalia mara ya mwisho tulivyokuja na leo unaona niwapongeze sana”, amesema Mhe Serukamba.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni; ujenzi wa mabweni, vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, bwalo, nyumba za walimu, miundombinu ya Barabara, ujenzi wa shule mpya za Makatapora, Itunundu, Ugwachanya, na Magunga, Pamoja na miradi ya maji.
Aidha Mhe. Serukamba amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Itunundu ambapo amepata fursa ya kuongea na wananchi wa Tarafa ya Pawaga sanjari na kupokea na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa