Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amewaasa wasafirishaji wanaopita kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa kufuata sheria ikiwa ni pamoja na kulipa kodi ya serikali na ushuru wa Halmashauri kwa mujibu wa sharia. Mkuu wa mkoa ameyasema haya alipo kuwa akikagua na kupata taarifa za vituo ya ukaguzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa 11 Desemba, 2023.
“Madalali wawe wakweli kwa wateja wao na kila mtu alipe kile anachostahili kwa sababu suala la kodi sasa hivi ni suala rafiki mnakaa mnazungumza, mnajadiliana baada ya hapo mmekubaliana huu ndio uhalisia mtu analipa” amesema.
Kuhusu suala la rumbesa, mkuu wa mkoa amesema suala hilo halikubaliki kisheria na kama mtu atabainishwa na kulipa faini, hiyo haimfanyi dereva aendelee na kosa lake kwa maeneo mengine bali anapaswa kurekebisha kosa lake.
Sanjari na hayo, Mhe. Dendego amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji (W) Wakili Bashir Mhoja na viongozi kutoka TRA kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya ukusanyaji wa mapato ya serikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Mhoja amefafanua changamoto za mara kwa mara zinazotoka kwa wasafirishaji kama ifuatavyo;
Vituo vya ukaguzi vilivyo tembelewa na kukaguliwa ni pamoja na kituo cha ukaguzi Migoli, kituo cha igingilanyi na kituo cha Wenda
Maeneo mengine ambayo Mkuu wa Mkoa ameyatembelea na kukagua miradi ni shule ya Msingi Migoli, na vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Tanangozi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa