Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda akimuwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) leo Septemba 5, 2024 amefunga rasmi Michezo ya Shirikisho la Michezo ya Serikali za Mitaa (SHIMISEMITA) katika Viwanja vya Nyamagana Jijini Mwanza.
Akizungumza na wanamichezo hao Mhe. Mtanda amesema serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuinua sekta ya michezo, sanaa na utamaduni na ni muhimu kwa watumishi wa serikali kumuunga mkono mchezaji namba moja nchini ambaye ni Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushiriki katika michezo hiyo iliyoandaliwa kwa ajili yao.
ezo mahala pa kazi inawajengea ari ya kuchapa kazi kwani ukamilifu wa afya inawajengea uwezo mkubwa wa kufanya kazi tena kwa weledi, huku mkiwaa mmeimarika wakati wote lakini pia yanawajengea uzalendo." RC Mtanda.
Aidha, amewataka wanamichezo hao kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za michezo ili malengo ya shirikisho hilo yatimie na ametumia jukwaa hilo kuzionya Halmashauri zilizokiuka taratibu na kupelekea kuondolewa kwenye michezo hiyo kuhakikisha hawafanyi hivyo tena kwani kuwapelekea watumishi kuwakosesha haki yao ya kujumuika na wenzao katika michezo.
Awali, Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Henry Kapela alibainisha kuwa jumla ya wanamichezo 2160 kutoka kwenye Halmashauri 100 wameshiriki mwaka huu tofauti na 45 za mwaka jana na kwamba uhamasishaji na maandalizi ya michezo ya mwakani unapaswa kuanza sasa.
Vilevile, ametoa rai kwa uongozi wa mashirikisho hayo ngazi ya Halmashauri kuzingatia taratibu na sheria za michezo chini ya shirikisho hilo ili kuwaepusha na usumbufu wa kuondolewa kama ilivyotokea kwa halmashauri 3 ambazo ni Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Dodoma na Manispaa ya Moshi.
Mshindi wa jumla wa michezo ya SHIMISEMITA kwa mwaka huu ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambao wamekua wa kwanza kwa michezo 9. Aidha michezo hiyo kwa mwaka huu imechagizwa na kaulimbiu isemayo "Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Taifa Endelevu".
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa