Akizungumza wakati wa kufunga maonesho ya Nanenane 2024 Kanda ya Nyanda za Juu kusini yaliyofanyika Jijini Mbeya Agosti 08, 2024 Mhe. Ridhiwani Kikwete Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu) kwa Niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema, katika Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 Serikali imedhamiria Kuendeleza sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuongeza Tija katika uzalishaji na thamani ya mazao.
“Serikali imeongeza Bajeti katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutoka Bilioni 275 mwaka 2021/2022 hadi Bilioni 295 MWAKA 2023/24 na Wizara ya Kilimo Bilioni 294 mwaka 2021/2022 hadi Trilioni 1.3 mwaka 2024/2025. Amesema Mhe. Kikwete.
Aidha amesema ongezeko hili la bajeti ni mahususi kwa ajili ya kuwezesha masuala ya utafiti na huduma za ugani lakini pia kutoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo, mifugo na uvuvi, kumarisha huduma za upimaji wa udongo na kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.
Pia Mhe. Kikwete amewaasa wakulima kutunza chakula ngazi ya kaya chakula ambacho kitawafikisha msimu mwingine wa mavuna na hivyo wauze kile ambacho ni ziada na kuzingatia lishe bora kwa watoto kuzuia ili udumavu.
Naye Naibu Waziri Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amesema kuwa wafugaji na wavuvi wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuga kisasa ili kupata tija na kuoneza kuwa hivi sasa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ndio unaoshauriwa na kazi hiyo imeanza ziwa Tanganyika na ziwa Victoria. Kwenye eneo hili la ufugaji wa kisasa Serikali ipo kutoa usaidizi juu ya ufugaji wa kisasa.
Maadhimisho ya Nanenane 2024 kanda ya Nyanda za Juu Kusini Jijini Mbeya yamehitimishwa Agoati 8, 2024 yakiwa na kauli mbiu, “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa