Viongozi wanawake wana uwezo mkubwa wa kushawishi jamii -DC Moyo
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Mohamed Hassan Moyo ameongoza Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 07/03/2022, ambapo imefanyika katika Kata ya Kalenga Kijiji cha Isakalilo.
Katika hotuba yake Mheshimiwa Moyo amejikita zaidi katika kauli mbiu ya mwaka huu inayosema: “Kizazi cha Haki na Usawa Kwa Maendeleo Endelevu, Tujitokeze Kuhesabiwa”, kwamba imebeba maanza nzito ya kukumbusha na kutenda haki inayoleta uwiano sawa kwa wanawake na wanaume katika ngazi za utoaji wa maamuzi na nafasi za Uongozi, lengo likiwa ni kuhakikihsa maendeleo yanaletwa na Watanzani wote bila ya kubagua ikiwa ni njia moja wapo ya kufikia Dunia yenye usawa wa kijinsia.
Mheshimiwa Moyo ameongeza kusema kuwa, Serkali inatambua kuwa, Wanawake viongozi katika nyadhifa mbalimbali wameonyesha kuwa ni hodara katika utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha Mheshimiwa Moyo amesema, katika kuhakikisha kuwa wanawake wanapata haki ya kumili Rasilimali, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kushirikiana na Wadau imewezesha zaidi ya wanawake 16,000 kupata hati miliki za kimila,
Pia Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 imtoa mikopo kiasi cha Tsh 328,000,000/= kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, lengo ni ikiwa na kuwainua kiuchuumi makundu maalumu na kufikia mlengo wa maendelo endelevu.
Mheshimiwa Moyo amemalizia kwa kutoa wito kwa wanume na wanawake kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la sense ya watu na makazi mwezi Agosti mwaka huu 2022, ambapo Serikali ya Tanzania hufanya sense kila baada ya miaka kumi, ikiwa sense ya mwishi ilifanyika mwaka 2012, hivyo sense ya mwaka huu itakuwa ni sense ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mheshimiwa Jackson Kiswaga, ameungana na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika maadhimisho hayo. Amemshukuru Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha ili kuboresha miundombinu katika maeneo yetu.
Pia Mheshimiwa Kiswaga ameongeza kusema kuwa, 80% ya uzalishaji katika jamii inatokana na wanawake, hivyo wajitokeze kwa wingi katika fursa mbalimbali pale zinapojitokeza ili kufikia lengo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa, ameshukuru kwa siku hii ya Wanawake Duniani na kusisitiza kusherehekea kwa Amani.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa