Kampuni ya HEMPEL Foundation ambayo inadhamini Shirika la SOS Childrens imetembelea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuona shughuli zinazotekelezwa katika miradi inayoendelea kwenye Kata ambazo wanazihudumia.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ni miongoni mwa Halmashauri 5 za Mkoa wa Iringa yenye shule 158 zikiwemo shule 153 za Serklai na 5 za Binafsi. Shule hizi zina jumla ya wanafunzi wapatao 75,995 wakiwemo wavulana 38,259 na wasichana 37,736.
Toka mwaka 2016 Shirika la SOS Childrens limekuwa likishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa katika kutoa huduma za elimu na uboreshaji wa kipato cha jamii katika Kata tatu za Nyang’oro, Malengamakali na Ulanda ambapo Shule nane za Msingi zilikuwa zikihudumiwa ambazo ni; kwa Kata ya Nyang’oro – Shule za Msingi za Chamndindi, Mawindi, Ikengeza na Holo. Kwa Kata ya Malengamakali ni Shule za Msingi za Iguluba, Makadupa na Isaka. Kwa Kata ya Ulanda ni Shule ya Msingi ya Ulanda.
Aidha shughuli zilizofanyika kutoka mwaka 2016 hadi 2022 ni kama kujenga maktaba mbiliza jamii katika vijiji vya Makadupa ambapo ipo Kata ya Malengamakali na Chamndindi ambapo ipo Kata ya Nyang’oro, pia kufanya ukarabati wa vyumba vya madarasa 20 katika shule zilizohudumiwa. Kuwasaidia watoto waliokosa nafasi katika mfumo rasmi wa elimu au kuacha shule kutokana na sababu mbalimbali, kujenga miundombinu ya kunawia mikoni ili kuwasaidia wananfunzi kuepuka maambukizi ya virusi vya korona.
Aidha, kuwapa walimu semina za umahiri wa masomo ya Lugha na Sayansi, pia kujenga madarasa na matundu ya vyoo kwa kushirikiana na wanajamii, na kufanya kuongezeka kwa umahiri wa masomo ya Lugha na Sayansi.
Mratibu wa Miradi hiyo Bwana David Mlowe amesema, “tumepata mafanikio mengi kutokana na ushiriano na Shirika la SOS Children, kama kupatikana kwa huduma za maktaba kwa jamii ambapo inawasaidia wanafunzi na jamii kujiongezea maarifa. Pia kuboreshewa mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji na kufanya mazingira ya shule na elimu kuwa bora, kupanda kwa ufaulu kwa wanafunzi katika mitihani ya Kitaifa, na kuimarika kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni kutokana na kuboreka kwa mazingira ya kujifunzia”.
Mlowe ameongeza kusema kuwa, “Shirikia hili limekuwa likiwalipa pesa ya posho kwa walimu wa kujitolea ili kuwaongezea ari ya kuendelea kufundisha watoto. Pia kupatikana kwa mahitaji ya wanafunzi wanatoka katika mazingira magumu na kuwafanya waipende shule na kutokata tamaa ya masomo”
Aidha mafanikio mengine ni ni kwa kupatika kwa vifaa vya TEHAMA kama vile kompyuta, prina nakadhalika. Pia kupungua upungufu wa madawati kutokana na utengezaji wa madawati mapya.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja, ametoa shukurani za dhati kwa Shirika la SOS Childrens kwa msaada uliotolewa ambao kwa kiasi kikunwa umeboresha utoaji wa elimu katika Halmashauri.
Wakili Muhoja amesema, “tunaomba Shirika la SOS Childrens kuendelea kushirikiana nasi katika utoaji wa huduam za keilimu ili kuinua kiwango cha ubora wa elimu katika Halmashauri”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa