Kwa Heri Stella Makali
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Stephen Mhapa ameongoza viongozi wa Halmashauri hiyo, viongozi wa Chama cha Mapinduzi, watumishi na wananchi mbalimbali katika kumsindikiza mtumishi Stella Makali aliyekuwa anahudumu Kitenga cha Sheria katika Halmashauri hiyo, ambapo alipata ajali na kupoteza maisha Novemba 02, 2023.
Bi Stella alipata ajali mapema asubuhi ya saa moja akiwa njiani kuelekea kazini, ndipo alipokutana na gari kubwa (Lori) uso kwa uso, akiwa katika gari yake lilimgonga na kupoteza maisha. Mazishi yalifanyika kijijini kwao Chipogolo Jijini Dodoma siku ya Jumamosi ya Novemba 04, 2023.
"Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe.... Amina!
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa