Taarifa ya Ilani ya CCM 2020-2024 Jimbo la Kalenga Yatolewa kwa Wananchi
Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kalenga wa kutoa taarifa ya Ilani ya Utekelezaji ya CCM 2020-2024 imetolewa mbele ya Wajumbe wa Kata zote za Jimbo la Kalenga na wananchi kwa ujumla. Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa Kichangani Julai 13, 2024
Akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa CCM Wilaya Komredi Costantine Kihwele amesema, anawashukuru wajumbe wote kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano huo na kwamba ni mara ya kwanza kwa Jimbo la Kalenga kusomewa utekelezaji wa Ilani ya CCM, hivyo ni muhimu kila mwananchi afahamu nini kinaendelea katika Jimbo lake.
Aidha Komredi Kihwele amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi za miradi katika Jimbo la Kalenga na miradi yote imetekelezwa na inaonekana, hivyo ni wajibu wa wananchi kumshukuru kwa kumpigia kura nyingi ifikapo wakati wa Uchaguzi Mkuu 2025.
Mgeni Rasmi katika Mkutano huo ni Mheshimiwa Livingstone Lusinde (Kibabji) ambeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa (MNEC), amewapongeza jimbo la Kalenga kwa kutekeleza Ilani ya CCM na kufanya mkutano kama huo kuwajulisha wananchi wake.
Naye Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mheshimiwa Jackson Kiswaga amewaomba wananchi kutobadilisha uongozi kwani kufanya hivyo ni kuchelewesha maendeleo. Pia amewaasa wananchi kutolinganishwa kwa viongozi wa muda mrefu na muda mfupi kwani uongozi unakuwa umetofuatiana sana kulinga na uzoefu, na maendeleo hayaji kwa siku moja tu.
Katika Mkutano huo Taasisi mbalimbali ziliweza kuwasilisha utekelezaji wake kama Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kutekeleza miradi mbalimbali kama ujenzi wa shule, zahanati, vituo vya afya, Hospitali, na miundombinu mbalimbali, TARURA, TANESCO, na Mamlaka ya Maji Vijijini (RUWASA).
Wananchi wamepokea kwa mikono miwili utekelezaji huo na kwamba wameahidi kutoa ushirikiano kwa kila hatua inayofanywa na Mheshimiwa Rais.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa