TAMISEMI na Benki ya Dunia Yatembelea Miradi ya SEQUIP
Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakiwa na Timu ya Benki ya Dunia wametembelea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kujionea miradi ya inayotekelezwa na Program ya SEQUIP katika ujenzi wa shule za sekondari mpya.
Program hii inatekelezwa kwa kujengwa shule za Weru iliyopo Kata ya Ulanda, shule ya Sekondari Mboliboli iliyopo Kata ya Mboliboli, Shule ya Sekondari Ifunda ambako kuna mradi wa Bweni na Shule ya Ufundi Ifunda ambako kuna mradi wa Bweni pia.
Kadhalika program ilianza kutekelezwa mwaka 2022/2023 kwa kujenga shule za sekondari Mlenge iliyopo Kata ya Mlenge na shule ya Sekondari Lufita iliyopo Kata ya Luhota.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa