Tamko la Afya na usafi wa Mazingira limetolewa katika kijiji cha Migoli wakati wa kampeni ya Mtu ni Afya iliyoongozwa na ndugu Mrisho Mpoto (Mjomba) iliyofanyika kijijini hapo Septemba 02, 2024
Kampeni ya Mtu ni Afya imebeba mambo muhimu ya msisitizo ambayo wananchi wote wamehamasishwa na kuelimishwa kupitia mkutano wa hadhara ulioambatana na michezo mbalimbali. Mambo yaliyopewa msisitizo ni; ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia, unawaji wa mikono, kutibu maji, ufanyaji wa mazoezi, hedhi salama, nishati safi, lishe, utunzaji na usafi wa mazingira.
Baada ya elimu na hamasa kutolewa kupitia michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta Kamba, rede, danadana na kuruka Kamba, wananchi wameulizwa na kukubali kubadilika na kuchukua hatua kwa tamko ambalo limetolewa na kaimu Mtendaji wa Kata ndugu Mlowe.
“Migoli ipo mbele kwenye suala la usafi wa mazingira na sasa tunaenda kurekebisha maeneo machache yaliyobakia lakini kwa upande wa hedhi salama kwa watoto wetu kama wazazi tunakaa nao vizuri na tutaendelea kuwa wasafi tunafanya kweli hatubaki nyuma” amesema Mhe. Yusta Kinyaga Diwani wa viti maalumu Migoli.
Kampeni hii imepambwa na kaulimbiu isemayo; FANYA KWELI, USIBAKI NYUMA “MTU NI AFYA”
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa