Timu ya Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Katibu Tawala (W), Mkurugenzi Mtendaji (W) na baadhi ya wataalamu ngazi ya Mkoa wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari Lufita na Mlenge 23.12.2023 ili kuhakikisha ukamilishwaji wa ujenzi wa shule hizo tayari kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 2024.
Pia kuna timu nyingine ambayo imeenda Kituo cha Afya Malengamakali kwa ajili ya kuhakikisha kuwa kituo cha Afya kinakamilika kwa Wakati.
Akiongea na Viongozi wa kata na vijiji pamoja na timu iliyofika kwa ajili ya usimamizi wa zoezi hili, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Mhe. Stephen Mhapa amesema “Kila mmoja atimize wajibu wake kwa sababu kazi hii ni suala mtambuka hivyo kila mmoja anahusika”
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa ndugu Michael Semindu amesisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano na kumtaka mhandisi ambaye ndiye focal person wa kazi hii kujua mahitaji ya kila jengo na kutoa taarifa kila siku ili kutokukwama.
Kazi tayari imeshaanza na dhamira ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kwamba hakuna wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza 2024 watakaokosa vyumba vya madarasa.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa