Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Ndg. Robert Masunya amewaasa watumishi kuhakikisha wanarithishana ujuzi walionao ili kuondoa utegemezi wa mtu mmoja katika Idara kuwa na uelewa wa kazi flani huku wengine wakikosa fursa hiyo.
Ndugu Masunya ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo kwa maafisa bajeti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa yaliyofanyika Octoba 01, 2025 katika ukumbi wa Siasa na kilimo yakiwa na lengo la kukuza uwezo wa maafisa bajeti katika uandaaji wa Mipango na bajeti za Idara na vitengo mbalimbali vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Ndugu Robert Masunya amesisitiza kuwa ni vyema kurithishana ujuzi badala ya kukumbatia maarifa na kwamba, watumishi wanatakiwa kupeana maarifa yatakayo rahisisha ufanyaji kazi katika taasisi.
"Katika taasisi zetu ni muhimu kugawana ujuzi ili Kila mmoja awe na uwezo wa kufanya kazi. Tusipende kukumbatia maarifa badala yake tufanye mambo kwa uwazi ili kutoa nafasi kwa wengine kujifunza na kuzifanya taasisi zetu kuwa Imara hata siku ikitokea waliokuwa na uwezo au ujuzi fulani hawapo basi sisi tunaweza kufanya kazi," amesema Ndugu Masunya.
Aidha ameongeza kuwa, washiriki wa mafunzo wanapaswa kuwa makini na kile wanachojifunza ili kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri mahali ambako mambo yalikuwa hayafanyiki vema na kwamba yale ambayo yamekuwa changamoto siku zote, ni wakati sasa wa kuhakikisha zinafanyiwa kazi.
Kwa upande wake Mtakwimu wa Halmashauri ya Wilaya ambaye pia ni Afisa Bajeti Ndugu Yahaya Kiliwasha amewahimiza washiriki wa mafunzo kuwa makini kupata uelewa ili waweze kuwa na uwezo wa kuandaa mipango na bajeti kwa usahihi kwa kuzingatia vipaombele, uwezo muda na shughuli husika au utekelezaji unaopimika na hatimaye kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa bajeti ikiwemo vifungu kubana.
Baadhi wa wajumbe katika mafunzo hayo wamepata nafasi ya kutoa shukrani zao kwa mafunzo huku wakiahidi utekelezaji wa walicho kipata katika mafunzo hayo.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa