“Tushirikiane Wazazi Wote Katika Malezi Ili Kuleta Ufanisi” – Robert Masunya
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Iringa Ndugu. Robert Masunya, amewaomba Wadau, Walezi na Wazazi kushirikiana katika malezi na makuzi ya watoto.
Ndugu Masunya amesema hayo leo Mei 21 alipokuwa anaongoza kikao cha Ulinzi na Usalama wa Mtoto na Mwanamke kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri wa Siasa ni Kilimo.
Ameongeza kusema kuwa, "ni vizuri wazazi kuwa karibu na watoto ili kuweza kufuatilia nyendo na kubaini tabia zao. Hata watoto wakiona wazazi wapo karibu ni rahisi wao kueleza changamoto wanazopitia”.
Pia wazazi ni vizuri kutoa elimu juu ya malezi kwa watoto wanaozaa kwenye umri mdogo ili wapate kujua haki na sheria zao.
Aidha, Ndugu Masunya amesema jamii ikubali mabadiliko katika kila jambo, kwani mawazo ya maana yanatoka katika jamii yenyewe na hatimaye inaweza kubadilisha Sera, na kwamba Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau na Mashirika mengine yasiyo ya Kiserikali katika masuala mbalimbali. Serikali ipo wazi muda wote kwa kupokea ushauri.
Pamoja na hayo, Katibu wa Kikao hicho Bi. Gladness Amulike aliweza kutumia kikao hicho kutambulisha Program Jumuishi ya Kitaifa (PJT) – MMMAM, ambayo ina mpango wa kutambua mtoto mwenye umri wa miaka 0-8 pamoja na mama.
Program hii inaanzia ngazi ya Kata hadi Taifa, ambapo inaangalia afya ya mtoto, malezi chanya, ujifunzaji, uchangamshaji, ulinzi na usalama wa mtoto ili mtoto aweze kukua vizuri. Katika hili Wadau mbalimbali wanahusika juu ya jambo hili.
Katika kikao hicho taarifa mbalimbali za Kisekta ziliweza kutolewa ambazo zimefanyika kwa kipindi cha Robo ya Tatu Januari – Machi.
Idara/Sekta zilizowasilisha taarifa zake za utekelezaji ni pamoja na Maendeleo ya Jamii, Elimu ya Awali na Msingi, Elimu Sekondari, TAHEA, Wawakilishi wa Vikundi vya Wanawake, SOS, Jeshi la Magereza, na World Vision.
Kadhalika Bi. Gladness aliweza kuwakumbusha wajumbe juu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, ambayo hufanyika Juni 16, ya kila mwaka, na kwamba kufanya maandalizi mapema.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa