Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amekabidhiwa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye Ulemavu toka kwa shirirka la IBO ITALIA, leo tarehe 06 Mei 2022.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya Tsh 18, 925,000 vimegawiwa katika shule mbalimbali zenye vitengo maalumu kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wenye ulemavu ambayo ni Kipera(Bweni), Kidamali, Kilambo, Luganga, Magozi, Nyerere Sec, Mgama pamoja na Kimande.
Akikabidhiwa mfano wa vifaa hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wakili Bashir Muhoja amelishukuru shirika hilo na kuwaomba kuendelea kufadhili Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuendelea kutoa huduma kwa wanafunzi wenye ulemavu
“Tunashukuru shirika la IBO ITALIA kwa kuendelez kufany akazi na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa bega kwa bega”.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la IBO ITALIA, Bi Paola Ghezzi amesema shirika hilo limekuwa likitekeleza mradi kwa mujibu wa makubaliano ya Wilaya ya Iringa kwa kiwango cha juu katika kusaidia sekta ya elimu na kwa kuwasaidia wanafunzi na watoto wenye ulemavu.
Naye Afisa Elimu Elimu Maalumu Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Wilfred Mattu amesema Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ina jumla ya wanafunzi wenye ulemavu 592 waliotawanyika katika shule mbalimbali za Msingi, kadhalika na Walimu Wataalamu wa Elimu Maalumu 27.
Pia nae ameshukuru shirika l;a IBO ITALIA kwa kufadhili ujenzi wa Mabweni ya kisasa, vyoo, ngazi mteremko, kununua na kugawa vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu, kununua gari kwa ajili ya wanafunzi wenye Ulemavu pamoja na kufanya uelewa kwa jamii kuhusu watoto wenye ulemavu
Shirika la IBO ITALUIA linasimamia kauli mbiu isemayo “NO ONE LEFT BEHIND” kwa maana ya kuwa hakuna mtoto yoyote anayetakiwa kuachwa nyuma katika suala la ujifunzaji na kupata mahitaji ya msingib katika maisha, kauli mbiu hii inaenda sambamba na kauli ya Sera ya Elimu inayosema “ELIMU KWA WOTE”.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa