Uwekezaji Mkubwa wa Serikali Umepelekea Ufaulu Mzuri – DC Kheri James
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Kheri James Julai 19, 2024 amekutana na Wakuu wa Shule na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya iliyopelekea matokea mazuri ya Kidato cha Sita 2024 katika Wilaya ya Iringa.
Akizungumza na Walimu hao katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo akiwa ameambatana Wakurugenzi wa Halmashauri Mhe. Kheri amesema kuwa, kutokana na Serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Elimu ndiyo jambo pekee lililopelekea matoka kuwa mazuri. Serikali imeboresha miundombinu kwa kujenga madarasa mpya, pia imeongeza walimu kwenye shule na kupandisha madaraja.
Pai Mhe. Kheri amesema kuwa, kutokana na matokea kuwa mazuri sasa ifike wakati kila mwananchi anakuwa na jukumu la kuhakikisha wananfunzi wanapata elimu bora ili kutokomeza ujinga katika Taifa letu.
Aidha, Mhe. Kheri ameaagiza viongozi wa Kata na Kijiji kuweka agenda ya elimu kuwa ya kudumu katika vikao vyao na wananchi katika suala la elimu.
Vilevile Mhe. Kheri amewaagiza Wakuu wa Shule kusimamia fedha zote zinazotolewa na Serikali kwa kuhakikisha miradi inakamilika na inaendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.
Nao Wakurugenzi wa Halmashauri akiwemo Mkurugenzi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa wamewapongeza Walimu hao kwa uchapakazi wao mkubwa wanaoufanya.
Wakizungumza mara baada ya kikao hicho baadhi ya Wakuu wa Shule wameseam kuwa, siri kubwa ya shule kupata matokeao mazuri kwanza ni miundombinu bora iliyowekwa kwenye shule hizo inayowanya wananfunzi hao kusoma kwa utulivu, na jambo lingine ni nidhamu ya wanafunzi.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa