Maafisa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki waaswa kufuata miongozo na maelekezo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kufanya kazi kwa unadhifu na haki. Hayo yamesemwa wakati wa kufunga mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura yaliyofanyika kijiji cha Migoli shule ya sekondari Nyerere Desemba 24, 2024.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Kalenga na Ismani ndugu Yahaya Kiliwasha amesema, “Someni kwa umakini sheria ya Uchaguzi, kanuni za uboreshaji, maelekezo na miongozo yoye inayotolewa na Tume ili kazi yenu ifanyike kwa unadhifu na haki”
Aidha ndugu Kiliwasha amesisitiza juu ya mawasiliano kati ya wataalamu hao na maafisa wa Tume upande wa TEHAMA ili ikiwa kutakuwa na changamoto ipatiwe utatuzi mapema na kuzinhatia muda kwenye kazi sanjari na huduma nzuri kwa wateja wanaokuja kwa ajili ya kujiandikisha.
Mafunzo yamefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 23 hadi 24, Desemba, 2024 ambapo jumla ya maafisa waandikishaji wasaidizi na waendesha vifaaa vya BVR 1000 wamepatiwa mafunzo tayari kwa ajili ya kwenda kuanza zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura linaloanza Desemba 27, 2024 hadi Januari 02, 2025.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa